Habari za Punde

*BLOG YA 'MBONGO' MISS JESTINA YASHINDA TUZO YA BLOG YA MWAKA UK

 Jestina (kushoto) akipozi kwa 'Snap' na mdogo wake Luiza, baada ya kupokea tuzo hiyo.
Mtandao wa SufUianimafoto na Urban Pulse Creative wanapenda Kumpongeza dada Jestina George, kwa kushinda tuzo muhimu ya Blog ya Mwaka katika tuzo za BEFFTA zilizizofanyika Jumamosi tarehe 22 Octoba 2011 ndani ya ukumbi wa Lighthouse, Camberwell jijini London.
Jestina akitoa Hotuba yake, alianza kwa kumshuru Mungu ambaye amemwezesha kumpatia uzima, afya njema pamoja na mafanikio makubwa aliyopata mwaka huu.

Aliendelea kwa kuwashukuru Wazazi wake na mwisho wadau wote ambao walimpigia kura Pia Mabloggers na Tovuti mbalimbali ambazo zimemsaidia kumpigia debe na kuibuka mshindi wa BLOG OF THE YEAR 2011 kutoka kwenye kundi lenye Blog 15 za kimataifa.

Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia katika kinyang'anyiro hicho, na kushinda na kuwa Mtanzania wa Kwanza kupokea tuzo za BEFFTA kwa upande wa Blogs.
Jestina George ameitoa wakfu Tuzo yake kwa dada yake mpendwa Kissa George ambaye ametangulia mbele za haki.
Vazi lake lilibuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania. Kwa maelezo zaidi na taswira mbalimbali za tukio hili Tembelea http://missjestinageorge.blogspot.com/
 Jestina akipozi na rafiki zake baada ya kupokea tuzo hiyo. kutoka (kushoto) ni Jacque Maina, Jestina George, See Li, Amina  Muussa na Zulfa Mussa.
 Frank Eyembe kutoka Urban Pulse, Lynn Kapinga, Jestina George, Mashel na Musa Sissasi Sarr.
 Zulfa, jestina, Lynn na Frank kutoka Urban Pulse wakifurahia ushindi.
Jestina akiwa katika pozi na Tuzo yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.