Select Menu

Habari

Burudani

Michezo

HABARI PICHA

Siasa

Videos

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa wafanyakazi akiwa kashikana mikono na Rais wa Jumuiya ya Vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Mh, Waziri wa Kazi na Ajira Mh Gaudence Kabaka (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh Galawa katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
 Gari la Kiwanda cha Cementi ya Simba, likipita mbele ya Jukwaa kuu, wakati wa maandamano ya magari ya viwanda yalipokuwa yakiingia uwanjani hapo.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Umati wa wafanyakazi na wananchi waliojitokeza katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wakiwa uwanjani hapo wakisikiliza Hotuba ya Rais Kikwete.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu kama zawadi kwa  Mfanyakazi bora wa Tanesco Bi Anetha Chengula  katika sherehe za Mei Mosi katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga leo.Picha zote na IKULU
 Mchezaji wa And 1 akifunga katika mechi dhidi ya kombaini ya mkoani Arusha.
 Mchezaji wa mpira wa Kikapu wa timu ya And 1 ya Marekani, akiweka saini katika Dayari za kumbukumbu za baadhi ya vijana wa Kibongo jijini Arusha baada ya kumalizika wa mchezo.
 Ay akipagawisha mashabiki waliojitokeza katika halfa ya kuwakaribisha wachezaji wa timu ya And 1 iliyofanyika jijni Dar es Salaam.
 Nemeless, akipagawisha jukwaani.
Wabongo wakipiga picha ya kumbuku na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
******************************
*Wapagawa katika tamasha la Coca Cola A Billion Reasons to Believe

Na Mwandishi wetu
TIMU ya mpira wa kikapu inayoundwa na wachezaji nyota wa zamani wa ligi ya Chama mpira wa kikapu cha Marekani American Basketball Association (ABA)  ijulikanayo kwa jina la AND1 imemaliza ziara yake kwa mafanikio makubwa huku ikiacha somo na gumzo kwa Watanzania kutokana na ujuzi walionyesha katika mchezo huo.

Andi 1 iliyokuwa chini ya mchezaji nyota, Dennis Chism maarufu kwa jina la Spyda iliweza kufanya mambo makubwa mkoani Mwanza na Arusha baadaye jijini Dar es Salaam na kuitandika Dar Dream team kwa 123-71.

Mbali ya Spyda, wachezaji wengine waliokuwepo katika ziara hiyo ni Phillip Champion Hotsauce, Robert Martin, Marvin Collins Highrizer, Brandon LaCue Werm, Jamar Davis, Alonzo Miles, Paul Otim na Justin Darlington.

Chism alisema pamoja na kuwashukuru wauzaji wa kinywaji cha Sprite kwa udhamini wao na kufanikisha kuja nchini, wamefuraishwa na jinsi wachezaji wa Tanzania waliovyoonyesha vipaji vyao. Alisema kuwa wachezaji hao wanatakiwa kuendelezwa ili kufikia hatua kubwa na hata kuweza kucheza ligi za kikapu za kulipwa Duniani pamoja na ile ya NBA.

Mbali ya kucheza, wachezaji hao walionyesha vipaji mbali mbali walivyonavyo katika kufunga pointi tatu, ku-dank na staili nyingine ambazo ziliwasisimua mashabiki wengi.

Baada ya kushiriki katika mechi za mpira wa kikapu, wachezaji hao walijumuika na watanzania wengine katika tamasha la muziki la Coca Cola A Billion Reasons to Believe  lililofanyika kwenye  ufukwe wa Mbalamwezi na kuona jinsi gani watanzania walivyokuwa wataalam katika muziki wa kizazi kipya na hip hop ambao asili yake ni Marekani ambako wao ndiyo maskani yao.
Wakali wa muziki kama Ambwena Yesaya (AY) na Nemeless kutoka Kenya walitamba katika tamasha hilo lililofana na kuwavutia mashabiki wengi.

 Wafanyakazi mbalimbali wa Serikali na Binafsi leo, wamejumuika kwa pamoja katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi iliyoadhimishwa leo Tanzania kote. Pichani ni wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakiingia kwa maandamano katika Viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa sherehe hizo leo.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa NHIF wakiingia kwa staili ya aina yake huku wakicheza sebene la Kiduku, na kufunika mbovu kwa sebene hilo latika maandamano.
 Wafanyakazi Mfuko huo wakisebeneka kwa pamoja katika maandamano hayo.
 Bendi ya Brass Band ya Magereza ikiongoza maandamano hayo, kuingia katika viwanja vya Mnazi Mmoja.
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakiingia na bango katika maandamano hayo.
 Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiingia kwa maandamano.
Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) wakiingia na bango katika maandamano hayo. Kushoto ni Suleiman (katikati) ni Neema, Idd na Jose Kongoro, wakiongoza maandamano hayo ya kundi lao.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Balozi wa Korea Kusini, Young Hoon Kim, kwa pamoja wakikata utepe kuzindua rasmi chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha VETA kilichojengwa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, wakati wa hafla ya ufunguzi wa chuo hicho iliyofanyika jana, mkoani Manyara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano:- wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Chuo kipya cha VETA, baada ya kufungua rasmi chuo hicho kilichojengwa Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara. Hafla ya ufunguzi wa Chuo hicho ilifanyika , mkoani Manyara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa ufundi wa Magari wa Chuo kipya cha VETA cha Mkoani Manyara, Treekta dogo linalotumika kulimia na kupandia Mbegu za mazao, wakati aliokuwa akitembelea na kukagua majengo mapya ya Karakana ya chuo hicho baada ya kukifungua rasmi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na viongozi wa Chuo cha Veta na viongozi wa Serikali baada ya ufunguzi rasmi wa chuo hicho uliofanyika, mkoani Manyara.