Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA PILI WA MWAKA WA WADAU WA PSPF

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bila, akiwa meza kuu na viongozi wengine walihudhuria ufunguzi wa mkutano Mkuu wa pili wa mwaka wa PSPF.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam. 
  Sehemu ya Wadau wa mkutano huo waliokuwapo ukumbini humo, wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Sehemu ya Wadau wa mkutano huo waliokuwapo ukumbini humo, wakimsikiliza Mhe. Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kitambulisho, Faridi Ibrahim Kiringi, mfanyabiashara wa duka la Nguo, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kitambulisho, Winfrey Ibrahim Banda, Mwalimu wa Shule ya Msingi, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa.
 Mzee Kssim Mapili, akishambulia jukwaa na wanamuziki wa bendi ya Mrisho Mpoto 'Mjomba Band' wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, ikiwa ni sehemu ya kutoa burudani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Hati na Nyumba na funguo, Adorat Francis Milinga, mmoja kati ya watu watano walionunua nyumba za PSPF, ambaye ni mmoja kati ya wanachama wapya wanaochangia kwa hiyari, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao na ishara ya ufunguzi wa mkuatano huo, uliofanyika leo Machi 7, 2013, katika Ukumbi wa jengo la Golden Jubilee Towers. Kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa. 
 Mzee wa Ndolelaga, akishambulia jukwaa wakati wa ufunguzi wa mkutano huo leo.
 Msanii, Mrisho Mpoto, akitoa burudani mbele ya jukwaa kuu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa pili wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), uliofanyika leo Machi 7, 2013 katika Ukumbi wa Jengo Golden Jubilee Towers, jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Fedha, Dkt. William Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na watumishi wa mfuko huo, baada ya kufungua rasmi mkutano Mkuu wa pili wa mwaka wa Wadau wa PSPF, leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.