Select Menu

Habari

Burudani

Michezo

HABARI PICHA

Siasa

Videos

Sheha wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said { Kidevu } wakati alipokuwa akipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban mwezi mmoja kabla ya kupelekwa Nchini India ambako ameanza uchunguzi na  matibabu zaidi. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
*****************************
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Miot Mjini Chenai Nchini India leo wanaanza kumfanyia huduma za matibabu Sheha wa shehia ya Tomondo  Mohd Omar Said { Kidevu } baada ya kukamilisha uchunguzi wa matatizo yake kufuatia kumwagiwa Tindi kali karibu mwezi mmoja uliopita.
Sheha Kidevu aliyefika Nchini humo Tarahe 21 na kufanyiwa vipimo vyote vilivyohusika anaanza matibabu kwa hatua ya kupandikizwa ngozi katika sehemu zake alizoathirika kutokana na kuungua kwa maji ya Tindi kali hiyo.
Akizungumza kwa njia ya Simu Daktari aliyeambatana  na Sheha huyo Dr. Said Ali Said { Mkarafuu } alieleza kwamba Madaktari wa India wameelezea kuridhishwa kwao na hatua kubwa iliyochukuliwa na Madaktari wa Zanzibar ya kumpatia tiba sahihi mgonjwa huyo.
Dr. Said alisema Madaktari hao Bingwa wa India wamekaririwa wakisema kwamba wamepata matumaini ya huduma hizo alizofanyiwa Zanzibar ambazo zinawapa hatua ya pili ya kuendelea na Tiba ya Sheha Kidevu.
“ Amefanyiwa  uchunguzi wa vipimo vyote na kubainika kwamba jicho lake Sheha Kidevu ambalo liliwahi kupata athari kidogo limewahiwa na Madaktari wa Zanzibar  wakiongozwa na Dr. Gang na Dr. Slim na hivi sasa liko katika hali ya kawaida “. Alifafanua Dr. Said Mkarafuu.
Alifahamisha kwamba Madaktari hao wa Hospitali ya Miot Mjini Chenai Nchini India wameelezea matarajio yao kwa mgonjwa huyo kuendelea na huduma za matibabu kwa haraka licha ya Madaktari hao kutokutaja huduma hizo zitamalizika katika kipindi gani.
Kabla Sheha Mohd Kidevu alikuwa akipatiwa huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kwa takriban Mwezi Mmoja sasa kutokana na kuathirika  sehemu ya kulia ya kifua chake, Bega pamoja na baadhi ya maeneo ya mapaja.
Sheha huyo wa Shehia ya Tomondo Mohd Omar Said Kidevu alipatwa na mtihani huo wa kumwagiwa Tindi kali { Acid }  na mtu asiyejuilikana Usiku wa tarehe 22 Mei Mwaka huu wa 2013 akiwa katika harakati za kuteka Maji mara baada ya kurejea kwenye Ibada ya sala ya Ishaa.
Vitendo vya matumizi mabaya ya tindikali vinavyofanywa na baadhi ya watu vinaonekana kuanza kuwatia hofu wananchi na hasa baadhi ya Viongozi katika maeneo mbali mbali hapa Zanzibar.
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy, akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za Baraza la Wawakilishi za mpira wa miguu na pete kutoka kwa Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt  Fimbo Mohamed Butallah, wakati wa makabidhiano yaliyofanyika kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto kwake ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan Juma. Picha kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited.
**********************************************
WAKATI HUO HUO:- MAANDALIZI YA TAMASHA LA GRAND MALT YASHIKA KASI ZNZ
Na Mwandishi Wetu
HUKU zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza, maandalizi yake yamezidi kupamba moto.

Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa tamasha hilo Jumatatu ijayo.

Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida.

“Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.

Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.

“Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.

“Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa  kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.

Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.

Wasanii wakali wa Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’na  Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii walioahidi kufanya kweli pia katika tamasha hilo.

Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Shrikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Cosmopolitan na Taifa Stars, Mathias Kissa (84) kilichotokea leo alfajiri (Juni 24 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani enzi zake, Kissa akiwa na timu ya Tabora alitamba katika michuano ya Kombe la Taifa wakati huo ikiitwa Sunlight Cup. Alikuwa akicheza katika nafasi ya ulinzi.

Baadaye alijiunga na Cosmoplitan ya Dar es Salaam, na pia kuwa mchezaji wa timu ya Taifa ambapo enzi zake akiwa na wachezaji kama Yunge Mwanansali wakiiwakilisha Tanganyika na baadaye Tanzania Bara walitamba katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati huo ikiitwa Gossage, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Kissa ambaye alipata tuzo ya mchezaji bora wa karne kwa upande wa Tanzania, tuzo inayotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) alikuwa ndiye mchezaji msomi kupita wote wakati akichezea timu ya Taifa akiwa amehitimu elimu ya Darasa la Kumi.

Kwa mujibu wa binti yake, Erica, marehemu ambaye pia aliwahi kuwa mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alioupata miaka mitano iliyopita, na kisukari. Baadaye alipata kidonda ambacho ndicho kilichosababisha kifo chake.

Msiba uko nyumbani kwa marahemu, Masaki, Mtaa wa Ruvu karibu na Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST). Maziko yatafanyika keshokutwa, Jumatano (Juni 26 mwaka huu) kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kisa, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Cosmopolitan na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Kisa mahali pema peponi. Amina
MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani. Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali duniani.

Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.

Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani. Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo litakaloendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika katika sehemu mbili.

Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja. Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa nyanja mbalimbali na kubadilishana nao mawazo.

Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa.

Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na waandishi wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata fursa ya kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza. “Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa mbali mbali.

Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa kufafanua umuhimu wa tamasha hilo kwa vijana.

Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na Majaji washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na Elena Kagan, Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene, Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican Karl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.

Taasisi ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina makao makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni kuendeleza maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha kuwezesha kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.

Taasisi ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye River huko Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi ina mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.
Benki ya NMB imefadhili michezo ya UMITASHUMTA katika Manispaa ya Sumbawanga kwa kutoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 9. Lengo kuu la ufadhili huo ni kusaidiana na UMITASHUMTA katika kuibua na kuendeleza  vipaji vya michezo kwa shule za msingi nchini Tanzania.
 Meneja wa NMB Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (kuli) akimkabidhi  Afisa Elimu, Modesta Zambi,  sehemu ya vifaa vya michezo vitakavyotumika kwenye michezo ya UMITASHUMTA  katika Manispaa ya Sumbawanga. Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kwenye manispaa hiyo.
Maofisa wa Benki  ya NMB  na maofisa wa Manispaa ya Sumbawanga wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB  Tawi la Sumbawanga, John Chinguku (tatu kulia)  wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vya michezo.

Sehemu ya mipira iliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili  ya UMITASHUMTA.
Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa TASWA, ambaye ni mwandishi wa habari wa gazeti la Daily News, Nelly Mtema amefiwa na mumewe usiku wa kuamkia leo. Msiba upo nyumbani kwake Kimara Matangini. Tutaendelea kupeana taarifa ya msiba huo.

Ahsanteni.
Katibu Mkuu TASWA
Na Mwandishi wetu
MASHINDANO ya Redds Miss Kanda ya Mashariki yanatarajia kufanyika Juni 29 Nashera Hotel mkoani Morogoro kwa kushirikisha jumla ya warembo 14.
Mkurugenzi wa kampuni ya Nikalex Ltd, Alex Nikitas aliwataja warembo hao ambapo wapo kambini hotel ya Starwing Hotel chini ya mkufunzi, Kudra Lupatu kuwa ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer ambao wote wanatoka Morogoro.
Warembo ambao wanatoka Mtwara kwa mujibu wa Nikitas ni Ivony Stephen (22), Purkeriah Ndovi (21), Zulfa Semboja (19) na wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainab Shaaban (23) na  Sophia Mganga (21). Wanaotoka mkoa wa Pwani ni Elizabeth Perty (22), Suleiyah  Abdi (22)  na Easther Albert (20).
Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge, Michuzi Blog, Clouds Media Group, Chilakale Resorts, Nashera Hotel, Starwing Lodge, Simple car Rental, Big Solution na Mikocheni Resort Centre yamekwisha kamilika na warembo watatembelea sehemu mbali mbali mkoa wa Morogoro na kufanya kazi za jamii.
“Tumejiandaa vziuri na warembo kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano hilo, warembo watatu wataiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya Redds Miss Tanzania ambayo yatafanyika mwezi Septemba,” alisema Nikitas.
Alisema kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutoka kwa warembo wote.
Naombeni msaada MABLOGER WENZANGU kuna mtu anaitwa Hansey Harrison/Hansey Harisonanatumia account mbili kwenye facebook nazo ni https://www.facebook.com/hansey.harrison?fref=ts
 na https://www.facebook.com/hansey.harison?fref=ts kanihack na pia anawatumia watu wangu sms kama ni mimi na kunichafulia kwenye account yangu ya facebook inayoitwa https://www.facebook.com/geofrey.adroph?ref=tn_tnmn na pia ananisumbua sana kikubwa nilikuwa nawaombeni mablogger wenzangu kuipublishi kwenye blog zenu ili iwe fundisho kwa wengine naombeni sana mnisaidie kwa hili ili iwe fundisho kwa wengine wanaotaka kuwachafua watu na pia namba yake ya simu ni 0712053949. HIZO JUU NI PICHA ZAKE

NI MIMI GEOFREY ADROPH WA PAMOJAPURE BLOG

Ndugu, Jamaa na marafiki wakijisevia msosi baada ya Bwana mdogo Fadhili Adam (wa tatu kushoto) kuchukua jiko jana, alipofunga ndoa huko maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam. Hongera Bwana mdogo kwa kuwaaga rasmi Makapera.
 Msanii wa muziki wa Kizazi kipya, Ben Paul, atakuwa ni miongoni mwa wakali watakaoangusha bonge la burudani katika shindano la Redd's Miss Temeke, Julai 5 mwaka huu.
 Wazee wa moja moja, Twanga Pepeta nao pia wataangusha bonge ya burudani katika shindano hilo.
********************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
MSHINDI wa tuzo ya utunzi bora wa nyimbo za bongo fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul amethibitisha na kukamilisha taratibu zote za kutumbuiza katika shindano la kanda ya Temeke, litakalofanyika Julai 5, katika ukumbi wa TCC Club Chang’ombe.
Ben Paul ambaye ni kipenzi cha mashabiki warembo kwa sasa, akiwa na anatamba na nyimbo lukuki zikiwemo Pete, Yatakwisha, Nikikupata na Waubani, atakuwa sambamba na bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta”, ambao itakuwa ni mara tu baada ya kuzindua albamu ya 13.

Shindano la Redds Miss Temeke, litakuwa linafanyika siku chache tu kabla ya mfungo wa Ramadhan, hivyo ni kama vunja jungu kwa wale wataoingia katika mfungo. Warembo 16 wamekuwa wakiendelea na mazoezi chini ya wakufunzi Suzan Mwenda na Shadya Mohamed.

Warembo hao ni pamoja na Aksaritha  Vedastus ,Irene Rajab, Darline Mmary, Esther Muswa   Hyness  Oscar, Latifa Mohamed, Jamila Thomas, Margreth Rajab, Magdalena Olotu, Mey Karume,Mutesa George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface, Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo.

Mashindano hayo yamedhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, City Sports Lounge, Blogu ya Wananchi, RIO Quality Gym &Spa, Fredito Entertainment na Kitwe General Traders. Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali.

Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.

Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 
2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. 

Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.

Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
Benny Kisaka
Mkurugenzi BMP Promotions
IMG_7558
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wakimbizi Dunia ambapo amesema anaishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani katika kuhakikisha Wakimbizi wanakuwa katika mikono salama ya Serikali ya Tanzania.
Kila tarehe 20 ya mwezi Juni Dunia inatambua uwepo wa mamilioni ya Wakimbizi Duniani katika kuhakikisha wanasaidiwa Ili kuondokana na hali ya Ukimbizi katika nchi za ugenini.
Aliendelea kusisitiza kwamba ni vigumu kuelewa Mazingira hatarishi ambayo mkimbizi anayapata kutokana na mapigano ya kisiasa, kidini au kikabila ambayo inawalazimisha kuhama katika makazi yao na kwenda katika makazi ambayo hawayafahamu, alisema watu wasiokuwa na makazi wanazidi kuongezeka Duniani mpaka 2012 takribani watu Milioni 3 walikuwa hawana makazi hizi ni kengele za uamsho wa Jumuiya ya Kimataifa kuamka na kuchukua hatua.
IMG_7577
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Pereira A. Silima akizungumzia majukumu ya Serikali katika kuwahudumia Wakimbizi kutoka nchi za jirani zenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika siku ya Wakimbizi Duniani jijini Dar es Salaam.
IMG_7542
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi Duniani (UNHCR) Bi. Joyce Mends-Cole akitoa nasaha zake ambapo amesema anatambua uwepo wa Shirika la Wakimbizi nchini Tanzania katika kuendeleza kampeni ya 2011 inayozungumzia umuhimu wa mwamko wa matatizo ya wakimbizi Duniani.
"Sisi Umoja wa Mataifa Tanzia tunasaidia kuhamasisha mwamko huo wa uelewa wa matatizo ya Wakimbizi katika Dunia ya utandawazi ili jamii ijue majanga na madhara ya vita katika familia na kaya".
Pia ameongeza kuwa Shirika la Wakimbizi Duniani litaendelea kuelimisha madhara ya vita katika nchi zinazoendelea ili kupunguza ongezeko la watu wasiokuwa na Makazi Duniani.
IMG_7569
Balozi wa Marekani nchini Mh. Alfonso Lenhardt na Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani Mh. Liberata Mulamula wakifuatilia hotuba mbalimbali katika siku ya Wakimbizi Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Juma.
IMG_7545
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo.
IMG_7547
Pichani Juu na Chini ni Wageni waalikwa na maafisa mbalimbali wa Umoja wa Mataifa nchini wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakijiri wakati wa maadhimisho hayo.
IMG_7603
IMG_7548
IMG_7546
Mkuu wa mkoa , Rehema
 Ujenzi wa barabara.
 Hii ni moja kati ya Mizunguko ya magari 'Round About' mpya zilizojengwa hivi karibuni mjini Dodoma, mzunguko huu unaoitwa Independence Square, upoa karibu kabisha na Soko Kuu la Majengo la mjini Dodoma, ambao kiukweli unavutia na unapendezesha mji. Hongera Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rehema Nchimbi, kwa juhudi zako za kupendezesha mji wa Dom na kutilia mkazo suala zima la usafi wa mazingira ambapo hivi sasa mji huu upo katika sura mpya kutoka na barabara nyingi za mitaani kuwekwa lami na kuondoa ama kupunguza usumbufu na karaha ya vumbi.
Wakazi wa zoezi la ujenzi wa Barabara za katikati ya Mitaa ya Manispaa ya Mji wa Dodoma, kuwa katika kiwango cha lami.
 Eneo hili ni Barabara inayopita mbele ya Soko Kuu la Majengo, ambalo bado halijafanyiwa ukarabati huo.
 Huku ni mtaani zaidi, Kinamama wakiwa na biashara zao za Chumvu wakisubiri wateja.
 Huu ni moja kati ya Mitaa ya Mji wa Dodoma, ambao tayari unameremeta kwa lami.
Pia mji huu bado unamagari kama haya mabasi ya kizamani yakiendelea kutoa huduma ya usafiri kama kawaida.
Hizi ni lugha za vyombo vya usafiri.....
Wachezaji wa Timu ya Spain, wakishangilia moja ya goli lao kati ya matatu dhidi ya Nigeria katika mchezo wao uliomalizika hivi punde ambapo Spain wameibuka na ushindi wa mabao 3-0
***********************************
TeamGPWTLGDPTS
BrazilBRA330079
ItalyITA320106
MexicoMEX3102-23
JapanJPN3003-50