Habari za Punde

*HATIMAYE AZAM WAANGUSHA 'MBUYU' YANGA NA KUTWAA NGAO YA AJAMII KWA MIKWAJU YA PENATI
Wachezaji wa Azam Fc, wakifurahi na kumrusha Kocha wao hewani baada ya kuibuka na ushindi kwa mikwaju ya penati 4-1 dhidi ya Yanga katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa leo jioni. Katika mchezo huo zilimalizika dakika 90 huku timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 na kuingia katika hatua ya matuta ambapo Azam walipata penati 4 na Yanga wakipata penati 1 iliyofungwa na Geigratius Munish 'Dida' huku Hassan Kessy na Haruna Niyonzima wakikosa.
***********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
HATIMAYE leo Azam Fc, leo wameibuka na ushindi wa mikwaju 4-1 ya penati na kunyakua Ngao ya Jamii kwa mara ya kwanza baada ya kuwafunga Yanga SC katika mchezo wa kuwania ngao ya Hisani uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. 
Hatua hiyo ya mikwaju ya penati imekuja baada ya timu hiyo kwenda sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90 huku Yanga wakiongoza mabao 2-0 yaliyofungwa na Donald Ngoma katika dakika ya 20 na 22 mabao hayo yalidumu hadi muda wa mapumziko na Azam Fc kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Shomari Kapombe dakika ya 74 akimalizia kazi nzuri ya Jean Baptiste Mugiraneza. na John Bocco, kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 90.


Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akimkabidhi Ngao ya Hisani Nahodha wa Azam FC, John Bocco baada ya mchezo huo kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa leo jioni.

********************************************
Penati hiyo ilipatikana baada ya beki wa Yanga Vincent Bossou kuunawa mpira mpira kwenye eneo la hatari.
Baada ya kumalizika dakika 90 timu hizo zilipigiana penati na Aishi Manula aliweza kupangua mkwaju wa beki Hassan Kessy huku Haruna Niyonzima, akipaisha.

Wachezaji wa Azam Fc wakishangilia na Ngao yao baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.

****************************************
Kipa Deo Munishi ‘Dida’ alifunga penalti pekee na ya kwanza kwa Yanga, wakati mikwaju ya Azam FC ikipigwa na John Bocco, Himid Mao, Shomary Kapombe na Kipre Balou. 
Ngoma alifunga bao la kwanza kwa penalti dakika ya 20, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na beki wa Azam FC, David Mwantika kwenye boksi.
Mwantika tena akafanya makosa yaliyoizawadia Yanga bao la pili dakika ya 22.
wakati akijaribu kumpiga chenga Amissi Tambwe, ikakataa na mshambuliaji huyo wa Burundi akaunasa mpira na kumpasia Ngoma aliyefunga bao la pili. 
Azam FC inatwaa Ngao ya Jamii kwa mara kwanza baada ya kuwania bila mafanikio mara nne kuanzia mwaka 2012 ikifungwa na Simba SC 3-2, kabla ya kuanza kufungwa mfululizo na Yanga 1-0 mwaka 2013, mwaka 2014 mabao 3-0 na mwaka jana kwa penalti 8-7 kufuatia sare ya 0-0.

Dakika chache tu baada ya kukabidhiwa Ngao hiyo, ilikuwa katika hali hii, kioo kwake na karatasi kwake....Duuuh ama kweli Ngao ya Jamii magumashi lukuki.

Aliyekabidiwa hata hajashuka jukwaani hali halisi ndo kama hivi je baada ya mwaka itakuwaje??????

Shughuli pevu ilikuwa ni kati ya Ngoma na Mwantika.....hapakutosha

Heka heka langoni kwa Azam Fc.....

Salum Abubakar akichuana na Amis Tambwe.

Beki Hassan Kessy akimtoka beki wa Azam Fc....

Juma Mahadhi akitiririka.....

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza 

Mashabiki wa Yanga baada ya bao la pili

Mbwembwe hizi ziliisha baadaye......
Mashabiki wa Azam wakiwa kimyaaaaaaa wakati timu yao ikiwa nyuma kwa mabao 2-0.
Baada ya muda na wao wakazinduka......

Mara na wao wakaanza kuanguka kwa presha.....

David Mwantika wa Azam Fc (kushoto) akiwani mpira na Donald Ngoma

Donald Ngoma akimtoka beki wa Azam FC, Ismail Adam

Shomari Kapombe akimdhibiti, Mwinyi Haji
Kipa wa Yanga Deogratius Munishi, akienda alijojo akipishana na mkwaju wa penati.
Kipa wa Azam Fc, Aish Manula akijaribu kuufuata mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima na kupaa juu ya lango
Wachezaji wa Yanga wakivishwa medali
Wachezaji wa Azam wakivishwa Medali zao na mgeni rasmi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.