Habari za Punde

*KAMANDA SIRRO KUWA MGENI RASMI PAMBANO LA NGUMI ZA KULIPWA KESHO

Mabondia Mfaume Mfaume kutoka Mabibo Nakos Camp (Kulia) akitunishiana misuli na Bondia Jonas Sego wakati wa zoezi la kupima uzito lililofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo Jijini Dar es Salaam.Mabondia hao watapambana katika mpambaono wa uzito wa kilogramu 64 utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Ndani wa Taifa.
 Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO)  Yassin Abdallah (Ustadh) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa zoezi la kupima uzito kwa mabondia Jonas Sego na Mfaume Mfaume watakao pambana kesho katika pambano la uzito kiligramu 64 litalofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.Wapili kutoka kulia ni Promota wa mchezo wa Ngumi Dotto Texas na Katibu Mkuu wa TPBO Ibrahim Kamwe (Big Right).
 Mwenyekiti wa Kamati ya muda ya Ngumi za kulipwa Tanzania Habib A. Kinyogoli akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa zoezi la kupima uzito kwa mabondia Jonas Sego na Mfaume Mfaume watakao pambana kesho katika pambano la uzito kiligramu 64 litalofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam. kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa TPBO Ibrahim Kamwe (Big Right), na Rais wa TPBO Yassin Abdallah (Ustadh).
 Bondia Jonas Sego akipima uzito kuelekea pambano lake dhidi ya Mfaume Mfaume litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Jonas alipata uzito wa Kilogramu 64.2.
Bondia Mfaume Mfaume akipima uzito kuelekea pambano lake dhidi ya Jonas Sego litakalofanyika kesho katika Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Jonas alipata uzito wa Kilogramu 64.0.
Promota wa mchezo mpambano baina ya Mabondia Jonas Sego na Mfaume (hawapo pichani) Mfaume akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi li upimaji uzito kwa mabodnia hao kukamilika leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Shija, Maelezo.
**************************************************************
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ngumi za kulipwa unaotarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa ndani wa taifa.

Hayo yamesemwa na Rais wa Tanzania Proffesinal Boxing Organisation (TPBO) Yassin Abdalla (Ustaadh) wakati wa upimaji uzito wa mabondia chipukizi wanaotarajiwa kucheza mchezo huo kesho tarehe 21/08/2016.

Amesema kuwa pambano hilo ni pambano bora nchini kwani linashirikisha wachezaji chipukizi ambapo mshindi wa pambano hilo ataandaliwa pambano la kucheza kiwango cha kimataifa la shirikisho la ngumiduniani (WBF).

Aidha, amesema kuwa pambano hilo litafuata sheria na taratibu za mchezo wa ngumi za kulipwa hivyo kuwaasa mashabiki na mabondia kuwa na nidhamu wakati wa pambano ili kuepukana na vurugu.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya ngumi za kulipwa Tanzania Habibu Kinyogoli amewaasa marefa watakaochezesha mchezo huo kuwa waaminifu, kufuata Sheria na taratibu za mchezo wa ngumi za kulipwa ili kupata mshindi kihalali.

Kwa upande wake Promota wa mchezo wa masumbwi nchini na mdhamini wa pambano hilo Bw. Dotto Texas amesema kuwa wachezaji wake wamejiandaa kwa pambano hivyo ameomba mashabiki wa Mchezo wa Ngumi kujitokeza kwa wingi katika Uwanja wa ndani wa Taifa na kuwataka wachezaji hao kuwa na nidhamu ili kulipa heshima pambano hilo.

Wachezaji wanaotarajiwa kupambana kesho ni Jonase Segu mwenye uzito wa kilo 64.2 kutoka Magomeni Kagera pamoja na Mfaume Mfaume mwenye uzito wa kilo 64.0 kutoka Mabibo Jijini Dare s salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.