Habari za Punde

*KAMATI YA UONGOZI YA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA YAKUTANA KUZUNGUMZA DAR

 Bi. Georgia C. Mtikila, Mjumbe wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
 Wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa wakati wa kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi wa Baraza hilo kilichokutana kujadili hali ya siasa Jijini Dar es Salaam.
 Bw.Constantine B. Akitanda, Mjumbe wa Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa     akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Secretarieti kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakifuatilia kwa makini wakati wa Kikao cha Kamati ya Uongozi.
*****************************************
Na Monica Laurent, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa wamekutana leo Jijini Dar es Salaam kujadili hali ya Siasa nchini.

Katika kikao hicho ambacho kilikuwa  cha dharura kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ,wajumbe wamekubaliana kwa pamoja kuwa, ipo haja ya kuitishwa kwa kikao cha Baraza la Vyama vya Siasa  kujadili hali ya siasa nchini.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Bw. Vuai Ali Vua ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa amesisitiza kuwa Kamati ya Uongozi inalo jukumu  la kuimarisaha na kudumisha  hali ya amani nchini pamoja na kujadili changamoto zilizopo katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi .

Aidha, wajumbe wa kikao cha Kamati ya Uongozi wameazimia kuonana na Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kwa lengo la kujitambulisha, kuelezea umuhimu wa Baraza la Vyama vya siasa  katika mfumo wa vyama vingi na kubadilishana mawazo  kuhusu hali ya siasa nchini.

Kamati ya Baraza la Vyama vya Siasa huundwa na Mwenyekiti  na Makamu Mwenyekiti wa Baraza ambao huchaguliwa na wajumbe wa Baraza, Katibu wa Baraza akiwa  ni Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye yuko kisheria na pia wenyeviti wa kamati nne za Baraza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.