Habari za Punde

*KAMERA YA MAFOTO KUTOKA BODA TO BODA YA LOITOKITOK

 HUKU kwetu inaruhusiwa tu!!!!, Dereva wa garo dogo akipakia mikungu ya ndizi kwenye gari lake kama alivyonaswa na kamera za Sufianimafoto mpakani mwa Tanzania na Kenya katika Boda la Loitokitok, akipakia mikungu hiyo ambayo hutoka mkoa wa Kilimanjaro nchini Tanzania.
 Dereva huyo akizdi kupanga mikungu hiyo kwa umakini ili iweze kuenea na kuanza safari ya kuelekea Jijini Nairobi.
 Mzigo umeshakaa tayari kwa safari...
 Dereva wa Baiskeli ya kubebea abiria, aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Abdi Mussa, akisubiri wateja katika Boda hiyo ambapo alisema kuwa hubeba abiria kwa Sh. 50 ya Kenya na huweza kujipatia kiasi cha Sh 215 kwa siku, lakini Abdi alisema kuwa ukihitaji Baiskeli hiyo anaweza kukuuzia kwa Sh 6800 ya Kenya.
 Pozi la kusubiri wateja....
 Eneo hili pia yapo magari madogo madogo yanayosubiri abiria kama daladala na dereva hukusanya nauli yake kabisa kabla ya kuanza safari kama anavyoonekana dereva huyu picha (kulia) akiwa na hela zake mononi.
 Magari hayo yakisubiri abiria
 Akitembea kusaka wateja wa suluali za Jeansi.
Akitembea kusaka wateja wa sweta na makoti.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.