Habari za Punde

*MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MENEJIMENTI YA OFISI YAKE IKULU KWA MAZUNGUMZO LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao kazi baina yake na watumishi wa Ofisi yake jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mh. January Makamba
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Mbarak Abdulwakil (kushoto) akiwa katika kikao kazi Ikulu jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bw. Richard Muyingi na Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Idara Mazingira.
 Baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati wa uwasilishaji wa mipango kazi waliojiwekea. Mawasilisho hayo yamefanyika hii leo Ikulu Dar es Salaam
 Sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Mh. Makamu wa Rais hii leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (wa kwanza kulia) akifuatilia mawasilisho ya mpango kazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam. wengine katika picha ni Katibu wa Makamu wa Rais Bw. Waziri Rajab na Katibu wa Waziri Bw. Anorld Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.