Habari za Punde

*MAVUGO ASHINDWA KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUFUNGA LEO, SIMBA IKILAZIMISHWA SARE NA JKT RUVU TAIFA

 Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo (kushoto) akichuana na beki wa JKT Ruvu Salim Gila, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0, huku mshambuliaji huyo akishindwa kufurukuta kwa mabeki wa JKT.
 Mavugo akijaribu kupiga shuti ambalo pia lilipaa juu ya lango.
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Burundi Laudit Mavugo, leo ameshindwa kufurukuta mbele ya mabeki wa JKT Ruvu  baada ya kushindwa kutimiza aahadi yake ya kuendelea kutupia nyavuni kama alivyo fanya katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ndanda Fc uliopigwa wiki iliyopita.
Mavugo alinukuliwa na moja kati ya gazeti  la michezo  nchini akitamba kuwa  baada ya kufanikiwa kupata bao lake la kwanza katika Ligi ya Tanzania bara akiwa mgeni, basi ataendelea kufunga kila mchezo atakaopangwa, ambapo leo ameshindwa kufanya hivyo timu yake ikilazimishwa sare na JKT Ruvu.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wa spidi kwa pande zote mbili huku timu hizo zikishambuliana kwa kushitukiza.

 MATOKEO YA MECHI NYINGINE LEO:
AZAM Fc 3- MAJIMAJI  0
MBAO FC 0- MADUI  1
RUVU SHOOTING  1- TANZANIA PRISONS  1
NDANDA FC  1- MTIBWA SUGAR  2
KAGERA SUGAR  0-  STAND UNITED 0
 Beki wa Simba Mohamed Hussein, akijaribu kuwatoka wachezaji wa JKT.
 Shizza Kichuya akichuana na mabeki wa JKT Ruvu.
 Jamal Mnyate wa Simba akichuna na beki wa JKT Ruvu.
 Toboooooooo
 Nahodha wa JKT Ruvu Michael Aidan (kulia) akiokoa moja ya hatari na kuumia hadi kutolewa nje baada ya kuumia mguu.
 Mshike mshike....
 Novalty Lufunga, akianguka na kuteguka mkono.
 Kikosi cha Simba
 Kikosi cha JKT Ruvu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.