Habari za Punde

*MAWASILIANO YABORESHWE KUELEKEA DODOMA

 Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TAGLA) Bw.Charles Senkondo wa kwanza kulia akimkabidhi kitabu cha maswala ya TEHAMA Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejemanti ,Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Bi.Susan Mlawi kushoto katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali uliofanyika jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ajira Daudi Xavier aliyesimama akiwasilisha mada mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejemanti ,Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Bi.Susan Mlawi hayupo pichani katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale akichangia mada katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali uliofanyika jijini Dar es salaam. Picha na Ally Daud-Maelezo
*************************************************
Na Sheila Simba-Maelezo
Mawasiliano ya TEHAMA yametakiwa kuboreshwa ili kusaidia Serikali katika mchakato wa kuhamia Dodoma kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ili kutekeleza mpango uliowekwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Akizungumza hayo katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha watendaji Wakuu wa Wakala za serikali (fcega) Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejemanti ,Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Bibi Susan Mlawi alisema kuwa mawasiliano hayo ya TEHAMA yanapaswa kupewa kipaumbele katika utendaji kazi wa serikali ili kupata watumishi bora.
“Matumizi ya teknolojia ya Tehama yatasaidia Nchi kufikia maendeleo haraka na kupunguza gharama za watu kusafiri kwa ajili ya kwenda kwenye vikao vya kazi kama zifanyavyo nchi nyingine” alisema Bibi Susan.
Aidha Bibi Susan ameongeza kuwa wakala wa serikali watumie mafunzo kwa njia ya mtandao(TAGLA)   kwa kuwa wana uwezo wa kutoa mafunzo yatakayoisaidia Serikali katika mawasiliano na taasisi zake hasa katika mkutano masafa(telle conference)
Mbali na hayo Bi. Susan amesema kuwa Kuongeza Ufanisi katika Mchakato wa Ajira kwa Kutumia Teknolojia” ni mada muafaka inayoleta chachu ya kuongeza  ubunifu na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi hususani katika taasisi za Kiserikali.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya ajira Daudi Xavier,alisema kuwa wanatumia teknolojia katika kupashana habari,upokeaji wa maombi ya ajira na utunzaji wa taarifa za waombaji fursa za ajira, katika kufanya mikutano ya kiofisi kwa kutumia mkutano masafa na kupunguza gharama za matangazo.
“Tunatumia Tehama sana katika kazi zetu na hii imetusaidia  kubaini wanafunzi wadanganyifu kwa upande wa vyeti kwa kufanya mawasiliano na taasisi za elimu kupata taarifa za watu wanaotuma maombi ya kazi”alisema Bw.Daudi.
Mbali na hayo pia  Mkurungezi Mkuu wa Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao(TAGLA) Bw.Charles Senkondo alisema kuwa lengo la kikao hicho ni kubadilishana mawazo na kutatau changamoto zinazozikabili taasisi mbali mbali za Kiserikali katika maswala ya teknolojia.
“Teknolojia sasa hivi imekua kwa kiasi kikubwa na tunaweza kutumia tehama katika kazi zetu za kila siku na sisi TAGLA tupo tayari kusaidia katika kuboresha hilo ili kurahisisha mawasiliano na kusaidia kujifunza teknolojia” alisema Bw.Senkondo
Kwa upande wake Mkurengezi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw. Hiiti Sillo alisema kuwa teknoloji hiyo isaidie katika kupata wakaguzi bora wa vyakula na dawa kwa maendeleo ya Taifa ili kusaidia jamii kuondokana na madhara yatokanayo na bidhaa zenye sumu.
“Naamini kupitia taaluma hii ya kisasa itasaidia sana katika kufanikisha ufanyaji kazi wetu katika kukagua na kuthibitisha bidhaa zilizo bora kwa matumizi ya watanzania”alisisitiza Bw.Sillo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.