Habari za Punde

*SIMBA YAANZA LIGI KWA MKWARA WA 3-1 DHIDI YA NDANDA FC TAIFA, AZAM YALAZIMISHA SALE NA AFRICAN LYON

Mshambuliaji wa Simba Laaudit Mavugo, akifunga bao la kwanza katika mchezo huo hii leo.
**********************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
TIMU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Ndanda Fc katika mchezowake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Laaudit Mavugo katika dakika ya 20 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki wa timu hiyo, Mohamed Hussein 'Tshabalala'.

Bao la kusawazisha katika dakika ya 37 lilifungwa na Omary Mponda kwa kichwa akimalizia krosi iliyopigwa na Nahodha Kiggi Makassy kufuyatia mpira wa adhabu ndogo.
Bao la pili la Simba lilifungwa na Mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Blagnon katika dakika ya 73 kipindi cha pili kwa kichwa akimalizia kona ya Tshabalala, huku bao la tatu likifungwa na Shizza Kichuya, akimalizia mpira wa Tshabalala baada ya mpira kutemwa na kipa wa Ndada Jackson Chove.

MATOKEO KATIKA VIWANJA VINGINE:
Azam Fc 1- African Lyon 1
Mtibwa Sugar 0- Ruvu Shooting 1
Stand United 0- Mbao Fc 0
Maji maji 0- Tanzania Prisons 1
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kupata bao la kwanza.
Shizza Kichuya akishangilia bao lake..
Heka heka langoni kwa Ndanda Fc.
Benchi la ufundi la Klabu ya Simba

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.