Habari za Punde

*SIMBA YAMRITHISHA MIKOBA YA UMENEJA MUSSA HASSAN MGOSI


Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
SHAMBULIAJI Mkongwe na nahodha wa timu ya Simba, Mussa Hassan Mgosi (Pichani)ametangaza rasmi kuachana na kusakata kabumbu na sasa anahamia upande wa benchi la ufundi, Mkongwe huyo amewahi tkucheza timu mbalimbali za ligi kuu kwa kujituma na kufikia malengo yake katika soka.

Mkuu wa kitengo cha Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Manara amethibitisha hilo na kusema Mgosi ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kwa kimataifa utakaopigwa Jumapili ya Juma hili uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya URA ya Uganda.

Manara amesema kuwa kwa sasa Mgosi atakuwa meneja wa timu na aliyekuwa Meneja wa timu, Abbas Suleiman Ally anakuwa Mratibu wa timu (Team Coordinator) huku kitambaa cha unahodha akikabidhiwa Jonas Gerald Mkude.

Aidha kiungo wa klabu hiyo, Peter Mwalyanzi aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea timu ya Mbeya City FC, ametolewa kwa mkopo African Lyoni liyopanda kucheza ligi Kuu msimu huu wa 2015/2016.

Inaelezwa mechi ya Simba na URA itakuwa ya mwisho ambapo Agosti 20 wekundu hao watashuka dimbani kukipiga na Ndanda wakuchelechele katika uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.