Habari za Punde

*UJIO WA MUIGIZAJI LUCY UWE CHACHU KWA MAENDELEO YA SANAA NCHINI

Msanii mkongwe nchini Ahmed Olutu (Mzee Chilo) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa kwa ajili ya uzinduzi wa igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika(Mrs. Lucy goes to Africa) jana Agosti 14,2016. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bw. Hassan Abbas (wa pili kulia) akifatilia igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa) wakati wa uzinduzi wa igizo hilo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016.
Baadhi ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa) likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess kwa kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kama vile Yvonne Cherly (Monalisa) na Suzan Lewis (Natasha) lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016.
Baadhi ya matukio katika igizo la Mama Lucy anakwenda Afrika(Mrs. Lucy goes to Africa) likiwa limeigizwa na Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess kwa kushirikiana na wasanii kutoka Tanzania kama vile Yvonne Cherly (Monalisa) na Suzan Lewis (Natasha) lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jana Agosti 14,2016.

Msanii kutoka Marekani Bi Toussaint Duchess(Mama Lucy) akiwashukuru wageni waalikwa na mashabiki mara baada ya kumalizika kwa igizo lake la Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa) lililofanyika jana katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Agosti 14,2016. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO
*****************************************************
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mkurugenzi wa Idara ya habari (MAELEZO) Bw. Hassan Abbas amesema kuwa ujio wa msanii wa maigizo kutoka nchini Marekani Bi. Toussaint Duchess maarufu kama Mama Lucy uwe changamoto kwa wadau wa sanaa nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa igizo la msanii Lucy linaloitwa Mama Lucy anakwenda Afrika (Mrs. Lucy goes to Africa) mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Abbas alisema kuwa ni vyema wadau wa sanaa wakatumia ujio huo kama changamoto itakayowasaidia kujifunza na kuwa wabunifu zaidi katika kazi zao za sanaa.
“Ujio wa muigizaji Lucy ni changamoto kwa wadau wa sanaa nchini, ni fursa ya kujifunza kwa wasanii hususani katika eneo la sanaa za jukwaani, vile vile ni fursa kwa vijana wa kitanzania ambao wanatarajia kufanya kazi za sanaa” alisisitiza Bw. Abbas
Aliendelea kwa kusema kuwa Serikali inatoa pongezi kwa kituo cha televisheni cha Azam na wasanii mbalimbali wakiwemo Suzan Lewis (Natasha) na Yvone Cherry (Monalisa) ambao wameshiriki kwa ubunifu wa kumleta msanii huyo nchini pamoja na maboresho mengine yanayofanywa na kituo hicho cha televisheni cha Azam.
Aidha, aliongeza kuwa akiwa Msemaji wa Serikali, anatarajia kushirikiana na wadau wa sanaa nchini kupitia mikakati mbalimbali itakayoandaliwa ili kuunga mkono juhudi aliyoanza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kujali na kusimamia kazi za sanaa na wasanii ili waweze kunufaika na kazi zao.
Kituo cha televisheni cha Azam kinatarajiwa kuonesha igizo hilo la msanii huyo kutoka nchini Marekani liloandaliwa kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali kutoka nchini wakiwemo Suzan Lewis (Natasha) na Yvone Cherry (Monalisa) pamoja na filamu mbalimbali zitakazofanywa na msanii huyo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.