Habari za Punde

*WANACHAMA YANGA WAOMBA MKUTANO WA DHARULA KUMFUTIA UANACHAMA MZEE AKILIMAI

 Baadhi ya wananchama wa Klabu ya Yanga wakiwa wamekusanyika nje ya Jengo la Klabu hiyo maeneo ya Jangwani leo asubuhi kwa ajili ya kuwashinikiza viongozi wao kuitisha mkutano wa dharula ili kumfutia uanachama Katibu wa Baraza la Wazee Mzee Ibrahim Akilimali, aliyesikika kwenye vyombo vya habri juzi akimshutumu Mwenyekiti wa Klabu hiyo,Yusuf Manji kwamba alikurupuka kutaka kumiliki timu hiyo.
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar.
BAADA ya jana kuzuka tetesi za Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kutaka kujiengua pamoja na kubadili msimamo wake wa kuikodi timu hiyo, wanachama wa klabu ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam wamempigia magoti na kumsihi asibadili maamuzi yake.
Wanachama hao wamemuomba Manji kutobadili msimamo wake leo katika kikao cha dharula kilichofanyika Makao Makuu ya timu hiyo maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Aidha wanachama hao wameikemea tabia ya baadhi ya viongozi wa timu hiyo kuzungumza na vyombo vya habari pasipo kupata ridhaa ya Klabu hiyo.
Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga Kanda ya Dar es Salaam, Robert Lyungu Kasera ameutaka uongozi wa timu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharula ili kupitisha pendekezo lao la kumvua uanachama katibu wa Baraza la wazee Ibrahim Akilimali kwa madai kuwa kiongozi huyo anashirikiana na timu pinzani kukwamisha mpango wa Manji kuikodi timu.
“Huyu mzee ana mikakati ya kuiharibu Yanga na hatufai, haiwezekani aongee masuala ya Yanga pasipo ridhaa ya uongozi wa klabu na viongozi mfikishe taarifa hii kwa usahihi bila kumun'gunya na kikao hiki kinalaani kitendo alichofanya,” amesema Lyunga.
Baada ya jana usiku baadhi ya wanachama kuzungumza na mtandao huu kuhusu sakata jilo leo asubuhi Mzee Akilimali, alisikika katika Kituo kimoja cha redio alichozungumzia juzi, akiwaomba radhi na kuwataka wanachama wa Yanga wasifikirie vibaya kwa kauli aliyoiongea kwani wao kama Baraza la Wazee wanamuhitaji sana Mwenyekiti wao Manji na ameweza kuisaidia timu yao kwa takribani miaka 10. 
"Labda niseme hivi Kama kukurupuka ni tusi kama nilivyomwambia Yusuf, basi naomba radhi kwake Manji na wanayanga wote”.
Kufuatia hilo Kaimu Katibu Mkuu Yanga amethibitisha kupokea pendekezo hilo ila amesema wao hawana uwezo wa kumfukuza mwanachama hadi mkutano mkuu ufanyike.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.