Habari za Punde

*YANGA YAPATA USHINDI WA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO KWA MO BEJAIA

 Winga wa Yanga Simon Msuva, akiruka kumiliki mpira wakati wa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi yao na Mo Bejaia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni. Katika mchezo huo leo Yanga wameweza kuibuka na ushindi wa kwanza tangu kuanza kushiriki michuano hiyo katika Kundi A baada ya kupoteza michezo iliyopita miwili na kutoa sare mmoja. Bao pekee la mchezo wa leo lilifungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 3.
**********************************
Na Ripota wa Sufianimafoto, Dar
BAADA ya Kupata ushindi wa kwanza katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Kocha mkuu wa Yanga, Hans Van De Pluijm, amesema ushindi huo umempa nguvu katika kuelekea mchezo unaofuata dhidi ya TP Mazembe.

Yanga imefanikiwa kushinda bao 1-0  lililofungwa na Mchezaji wa kimataifa kutoka Burundi, Amis Tambwe katika dakika ya tatu dhidi ya Mo bejaia mechi iliyochezwa dimba la uwanja wa Taifa.
Pluijm amesema kuwa, wachezaji wake wamecheza vizuri sana na wameweza kulinda goli katika dakika zote ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza ila anawapa hongera kwa jitihada walizozifanya hadi kupata bao hilo, pamoja na wachezaji wake kukosa mbao mengi ya wazi.

Naye Nahondha wa Yanga, Vicent Bossou amesema wamefanya kazi kubwa katika kuhakikisha wanatoka na ushindi pamoja na kuwa wamecheza timu nzuri na yenye uzoefu wa muda mrefu wa michuano ya kimataifa ila anawapongeza pia wachezaji wenzake kwa juhudi na kujituma katika mchezo huo.

Baada ya ushindi huo Yanga wanaendea kusalia katika nafasi ya nne wakiwa na alama nne huku wakibaki kuomba dua mbaya kwa wenzao wa Medeeama wanaokipiga kesho na Mazembe kesho nchini Ghana.
Sehemu ya Mashabiki wa Yanga waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.