Habari za Punde

*ASHANTI UNITE YAITANDIKA PAMBA FC BAO 1-0 MBIO ZA KUREJEA LIGI KUU BARANa Mwandishi Wetu,Dar
TIMU ya Ashanti United leo imeanza mbio za kuwania kujerea ligi kuu Bara baada ya kuifunga Pamba FC, bao 1-0, kwenye Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo kila timu ilianza kucheza kwa tahadhari huku kila mmoja akijaribu kushambulia lakini Ashanti United ndio ilifanikiwa kupata bao dakika ya 41 lililofungwa na Abeid Kisiga akiwa nje ya eneo la 18 kwa shuti kali.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko ambayo yaliisaidia Pamba kuliandama ango la Ashanti kwa kipindi chote lakini mabeki na kipa wa Ashanti walifanya kazi nzuri kwa kuondoa hatari zote.

Akizungumza na Mtandao huu baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa Ashanti United, Maalim Swalehe alishukuru kwa ushindi mwembamba waliopata na kuwatupia lawama wachezaji wake kuwa wamecheza chini ya kiwango.

“Nashukuru tumepata pointi tatu lakini wachezaji wameniangusha kwa sababu wamecheza tofauti na maelekezo yangu hali iliyosababisha mchezo kuwa mgumu kwani tulikuwa na uwezo wa kushinda zaidi ya mabao tatu.

Mchezo unaofuata kesho ni Coastal Union na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Mkwakwani na Kimondo dhidi ya Mbeya Warriors Uwanja wa Vwawa. 

Jumatano Septemba 26, 2016 Mshikamano itacheza na Friends Rangers kwenye Uwanja wa Karume wakati Jumanne kwenye uwanja huohuo Polisi Dar itacheza na Kiluvya Utd.
Sehmu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.