Habari za Punde

*CCBRT YAZIDI KUIMARISHA HUDUMA KWA WATOTO WACHANGA

Dr. Mchomvu kutoka CCBRT (kushoto) akishirikiana na madactari wa muhimbili katika wodi ya watoto  kukamilisha zoezi la uwekaji wa vifaa vya kuokoa maisha ya watoto wachangaDactari bingwa wa watoto katika hospitali ya Muhimbili Dr.Majaliwa (katikati) amefurahishwa sana na jitihada zinazofanyika kupitia hospitali ya CCBRT kupambana na tatizo la vifo vya watoto wachanga.Kupitia mpango wa kutoa mafunzo ya Uzazi na vichanga(Maternal & Newborn) unaofanya kazi kwa wasaidizi wa Afya kwenye vituo 23 katika mkoa wa Dar es salCCBRT imeanza rasmi jitihada zake za kuhakikisha inapunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na wanozaliwa kabla ya muda kwa kutoa msaada  wa vifaaa vya kuwasaidia watoto wachanga .Mpango huu umewezehswa na Vodacom Foundation,Jitihada hizi zitatoa vifaa maalum   ambavyo vitatumika kuwasaidia wauguzi katika utatuzi wa matatizo yanayosababisha vifo vya watoto wachanga,watoto wanozaliwa kabla muda ya muda(pre maturity)wanaozaliwa na maambukizi na na wanozaliwa  na tatizo la mfumo wa hewa na jambo la msingi kabisa ni kushiriki katika harakati za kupunguza vifo vya watoto wachanga katika mkoa wa Dar es Salaam.
Vifaa hivyo  vimegharim jumla ya dola za kimarekani 90,000 kwa  ajili ya ununuzi wa vifaa hivi vya kusidia kuokoa maisha ya vichanga.Na zoezi hili  litafanyika katika wodi 4 zinatoa huduma kwa watoto wachanga katika mkoa wa Dar es Salaam na tayari limeanza  rasmi katika hospital kuu ya rufaa Muhimbili na linaendelea katika hospital ya Temeke Mwananyamala na Amana.
Mafunzo kwa ajili ya matumizi ya vifaa hivyo yataanza kutolewa mapema wiki ijayo ambayo pia yamefadhiliwa na Vodacom Foundations.Wataalam wa kiufundi waliotengeneza vifaa hivyo  pia watakuja kutoa mafunzo kwa madaktari wa watoto wachanga kuhusu jinsi ya kuvitumia na kuvitunza vifaa hivyo pia kwa makampuni ya kitanzania kwa ajili ya urekebishaji kama vikipata hitilafu.
CCBRT pia inamiliki hospital ya Wazazi na Watoto wachanga ambayo itafanya kazi kwa ukaribu sana na hospitali za rufaa za mkoa wa Dar es Salaam ambayo itajikita sana  na dalili hatarishi wakati wa kujifumgua.Hospital hii itaanza rasmi kuanza kufanya kazi mnamo mwaka 2018.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.