Habari za Punde

*KANDANDA DAY KUCHANGIA MADAWATI KUFANYIKA OKTOBA 15

TAMASHA la Kandanda maarufu kama ‘Kandanda Day’, linatarajia kufanyika Oktoba 15, mwaka huu katika kiwanja cha Jakaya Kikwete Park (zamani Kidongo Chekundu).
Katika tamasha la mwaka huu,kauli mbiu itakuwa ni ‘Mpira na Dawati’,kwa maana ya tamasha hilo kutumika kukusanya fedha kwa ajili ya kununua madawati yatakayogawiwa kwa shule mbalimbali nchini.
Mratibu wa tamasha hilo,Mohamed Mkangara,amesema kwamba mwaka huu wameamua kuja na kauli mbiu hiyo, ili kuunga mkono kampeni inayoendelea ya Serikali kuhusu madawati kwa shule za msingi na sekondari.
“Umekuwa ni utaratibu wetu kila mwaka huu,kuja na kauli mbiu ambayo itahusisha soka na jambo ambalo moja kwa moja linaihusu jamii,kwahiyo, tumeona kwa kutumia soka,tunaweza kuisaidia jamii yetu kwa urahisi,”alisema Mkangara na kuongeza:
“Ndio maana kwa miaka yote tuliyofanya tamasha letu,kumekuwepo na ‘impact’ ya moja kwa moja kwa jamii inayotuzunguka,kwa hiyo ule utamaduni wetu tuliokuwa nao kwa miaka minne tunaendelea nao kwa mwaka huu kwa kukusanya fedha kwa ajili ya manunuzi ya madawati,ambapo tunatarajia kuchangisha fedha na kuuza jezi katika ‘dinner’ maalum ambayo tumeandaa kwa wadau mbalimbali.”
Mkangara,alisema kwamba madawati ambayo yatapatikana yatagawiwa kwa wawakilishi waliochaguliwa wa Kandanda kutoka mikoa mbalimbali nchini, ambao watahudhuria siku hiyo.
“Tamasha letu kila mwaka linakua na wigo unazidi kuwa mpana,kutokana na kushirikisha wadau wa mikoani,hivyo,kwakuwa hili jambo ni la kitaifa,tumeamua kama kamati kugawa madawati kwa wawakilishi wetu wa mikoani ambao tunatarajia watashiriki tamasha letu,huku tukiwaomba wadau wengine watuunge mkono katika kampeni yetu,”alisema Mkangara
Tamasha la mwaka huu linatarajia kushirikisha timu mbalimbali alikwa,ukiacha timu wenyeji Time Dizo Moja na Timu Ismail.Pia,tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali na michezo ya kuvuta kamba kwa washiriki.

Imetolewa na Mratibu wa tamasha
Kandanda Day
Mohamed Mkangara
Mobile: 0713299631

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.