Habari za Punde

*KIJITONYAMA VETERANS KUKIPIGA NA WARIOBA VETERANS, SINZA VETERANS

 Kikosi cha Kijitonyama Veterans
Kikosi cha Warioba Veterans
***************************************
Na Mwandishi wetu, Dar
Timu ya Kijitonyama Veterans, kesho Jumapili, itapambana na timu ya Warioba Veterans katika mchezo wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Kijitonyama maarufu kwa jina la uwanja wa Bora au “Emarates”.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 asubuhi na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mratibu wa timu ya Kijitonyama Veterans, Majuto Omary.
Mbali ya mechi hiyo ya asubuhi, Kijitonyama Veterans pia jioni itapambana na timu ya Sinza Veterans katika mchezo mwingine wa kirafiki uliopangwa kufanyika kwenye uwanja huo huo.
Majuto alisema kuwa mechi zote mbili  ni sehemu ya kujiweka fiti kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya ligi ya timu za veterans iliyopangwa kuanza baadaye mwezi huu kwa  Manispaa ya Kinondoni. 
Alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya mechi hiyo na kuahidi ushindi.
“Tupo vizuri kwa ajili ya mechi zote mbili na hii inatokana na kuwa na kikosi kikubwa ambacho , tumejiandaa vyema na tunaahidi kufanya vyema katika mchezo huu,” alisema Majuto.
Kocha mchezaji wa timu ya Warioba Veterans, Barnabas Emilio alisema kuwa wamejiandaa kulipa kisasi kwa Kijitonyama Veterans ambao katika mechi ya mwisho walifungwa mabao 3-0.
“Tumedhamilia kulipiza kisasi katika mchezo huo, tunajua utakuwa mgumu, ila tumejiandaa kwa ajili ya mechi hiyo na ushindi ni lazima,” alisema Barnabas.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.