Habari za Punde

*KUTANA NA KIJANA AZIZ MAKOROKOCHO ANAYEJITOA KUSAIDIA JAMII KULIKO UWEZO WAKE

Kijana Azizi Habb,mkazi wa Ubungo National Housing jijini Dar es Salaam, akipaka rangi biashara yake ya magari ya kuchezea watoto kwa ajili ya kuandaa kuuza kwa wateja wake eneo hilo. Azizi amebuni biashara hiyo inayomuingizia kipato kidogo ambacho pia ameamua kukigawa kwa kujitolea kuwasaidia Jamii eneo analoishi. Aziz kama alivyokutwa na kamera ya Mafoto akiwa katika shughuli zake aliweza kuzungimza na Mafoto Tv na kueleza vile anavyojitolea kuwasaidia wananchi wa mtaani kwake na hata wapita njia wasiofahamiana.

Katika mtaa huo Azizi amejenga Daraja linalotumiwa na wakazi wa eneo hilo na hata wapitanjia pasi kujua nguvu, gharama na akili iliyotumika kama ni ya kijana huyu aliyeamua kufanya kwa kujitolea pasipo kusaidiwa na mtu.

Baada ya kukamilisha ujenzi huo Aziz aliamua kuweza kibakuli darajani hapo ili kila anayeguswa na jitihada zake aweze kuchangia chochote pasi kulazimishwa, lakini cha ajabu ni kwamba wengine huthubutu hata kumtusi kijana ahuyo anapokuwa katika harakati za kuhamasisha ''jamani kutoa ni moyo''. 

Aidha Aziz alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo ulimchukua miezi mitatu hadi kukamilika kutokana na kukusanya nguzo, mbao, misumari taratibu kulingana na kipato chake na kuwalipa vijana wenzake ili kumsaidia kupandisha nguzo hizo za Tanesco ili kuanza kujenga. Anasema Daraja hilo liligharimu kiasi cha Sh. zaidi ya 700,000, huku vijana wenzake akiwalipa kiasi cha sh. 150, 000 kumsaidia kupandisha nguzo juu ya kuta ili kuanza ujenzi.

Cha kushangaza sasa kwa kijana huyu, ni kwamba yeye ameamua kujitolea zaidi kwa watu kuliko kujisaidia yeye binafsi kwani kwa gharama hizo angeweza hata kuboresha ofisi yake hii lakini akaamua na bado anamua kujitolea kusaidia jamii zaidi, kwani mpaka sasa bado anafikiria kuendelea kuboresha daraja hilo kwa Chuma ama Zege ili wananchi waweze kuendelea kutumia daraja hilo kwa amani na bila wasiwasi.

''Natamani siku moja nipate hela na uwezo wa kulijenga daraja hili kwa Chuma ama Zege ili hata siku moja nikifa,wananchi wabaki na kumbukumbu yangu kuwa niliwasaidi, hivyo Daraja litabaki kama kumbukumbu yangu mahala hapa'', alisema Aziz

USIKOSE MAHOJIANO KWA KUBOFYA MAFOTO TV ONLINE HAPA HAPA  www.sufianimafoto.com, AMA YOUTUBE Muhidin Sufiani
 Azizi akiandaa biashara yake tayari kwa kumkabidhi mteja wake.
 Gari likitestiwakabla ya kukabidhiwa mteja
 ''Tayari liko sawa mama unaweza kwenda''
Mteja akikabidhiwa gari lake
Aziz anasema kuwa kazi yake hiyo humchukua siku moja kutengeneza gari moja hadi kukamilika, hapa akipaka rangi baada ya kukamilisha matengenezo yaani kuunga.
Maandalizi yakiendelea

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.