Habari za Punde

*LIGI YA WANAWAKE MPIRA WA MIGUU KUANZA KUTIMUA VUMBI MWEZI HUU

Mwenyekiti wa soka la wanawake Amina Kaluma akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na semina elekezi kwa timu za wanawake zinazotarajia kushiriki ligi kuu ya wanawake itakayotimua vumbi hivi karibuni, (Kulia) Ofisa habari wa Shiriksho la Mpira wa Miguu TFF Alfred Lucas na Makamu Mwenyekiti wa Soka la wanawake Rose Kisiwa (Kushoto). 
**********************************
Na Zainab Nyamka, Dar
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeandaa semina elekezi kwa klabu za Ligi Kuu za wanawake inayotarajiwa kuanza baadaye mwaka huu.
Semina hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo, itafanyika Jumamosi Septemba 3 mwaka huu ikiwa ni kwa ajili ya kuwapa maelekezo mbalimbali na kanuni.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake , Amina Kaluma pichani kushoto,amesema kuwa hii ni moja ga fursa itakayosongesha mbele soka la wanawake nchini.
Kaluma amesema kuwa makocha wote pamoja benchi la ufundi watapewa semina elekezi kuhusu kanuni za ligi, usajili wa timu na taratibu nyingine za ligi hiyo ikiwa ni pamoja na sheria za mpira wa miguu ambazo zimekuwa na marekebisho kwa msimu wa 2016/2017 kama zilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kaluma amesema ligi hiyo itaanza kwa mfumo wa makundi mawili ambao katika kila kundi zitatoka timu tatu zitakazocheza na kupatikana kwa mshindi wa kwanza, pili na tatu.
Timu zitakazoanza kushiriki ligi mwaka huu ni Viva Queens ya Mtwara, Fair Play FC ya Tanga, Panama FC ya Iringa, Mlandizi Queens ya Pwani, Marsh Academy ya Mwanza, Baobao Queens ya Dodoma, Majengo Queens ya Singida, Kigoma Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queen pamoja na JKT Queens, Mburahati Queens na Evergreen Queens za Dar s Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.