Habari za Punde

*MATUKIO KATIKA PICHA JIJINI DAR LEO,JAMAA ANASWA BENKI YA NBC KIMSHANGAO

Askari Polisi aliyevalia kiraia (kulia) akimdhibiti raia ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja (kushoto) nje ya jengo la Makao Makuu ya Benki ya NBC Posta ya zamani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. Haikuweza kufahamika kwa haraka chanzo cha jamaa huyo kutiwa nguvuni na askari hao waliompakia kwenye gari lao la Doria na kuondoka naye mahala hapo.
Jamaa huyo akidhibitiwa na askari 
wa kampuni ya Ulinzi ya SGA  na Askari Polisi wanao linda Benki ya NBC maeneo ya Posta ya zamani Jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa Jamaa huyo alishuka katika gari lenye namba za usajiri T 
662 BUK kablaya kuzuka varangati hilo.
Akipelekwa kituo cha polisi baada ya kudhibitiwa

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.