Habari za Punde

*MBUNGE PETTER MSIGWA AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI, AKABIDHI MADAWATI 537 KWA AJILI YA JIMBO LA IRINGA MJINI

MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 ambayo ameyatoa kwa ajili ya jimbo la iringa mjini.
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe 
haya ni baadhi ya madawati 537aliyokabidhi MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msingwa
****************************************** 
Na Fredy Mgunda, Iringa
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa amekabidhi madawati hayo 537 ambayo ameyatoa katika jimbo lake yataweza kuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuweza kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya kusoma katika mlundikano mkubwa na baadhi yao walikuwa wanakaa chini ya sakafu.

Aidha Msigwa katika hotuba yake ya kukabidhi madawati hayo amewataka viongozi wa manispaa ya iringa na tabia ya kuhujumu na kuiharibu miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za serikali kwa lengo la kuweza kuwasaidia watoto wengine wa vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.

“Sipendi kuona wanafunzi wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini,kitendo hicho huwa kinaniumiza sana ndio maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili kufanikisha adhima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la iringa mjini”alisema Msigwa

Naye meya wa halmashauri ya manispaa ya iringa Alex Kimbe amesema kwamba kwa sasa hawana mapungufu yoyote ya madawati hivyo hakutakuwa na changamoto ya mwanafunzi wake kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu.

MADAWATI hayo 537 ambayo yametolewa na ofisi ya Mbunge wa Iringa Mjini yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 60 yatasambazwa katika kata zote ambapo pia yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea adha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo kwa kipindi cha muda mrefu na hatimaye kuongeza kiwango cha ufaulu.

Lakini tatizo la kupanda na kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika baadhi ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya manispaa ya iringa lilikuwa linasababishwa na wanafunzi wengine kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu sambamba na kuwepo katika mazingira ya miundombinu ambayo sio rafiki kwao hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari na shule za msingi katika manispaa ya iringa.

Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph,Paul Kisige pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa sakafuni kimepelekea kupunguza uwezo wa kifikiri na kujikuta wanafanya vibaya katika masamo yao na kushindwa kufaulu, hivyo wamempongeza mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji Petter Msingwa kwa juhudi wanazozifanya za kupambana na adha ya madawati.

“Hapo mwanzoni kwa kweli hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma wakiwa wanakaa chini ya sakafu na hii kiukweli unamwondolea kabisa uwezo wa kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu kubwa na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu, na pia tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,”walisema wanafunzi hao.

Pia walisema kwamba pamoja na changamoto ya kuwepo kwa upungufu wa madawati lakini serikali inatakiwa kuhakikisha inatilia mkazo suala linguine la nyumba za walimu pamoja na kuimarisha mambo mengine ya msingi, kama kuongeza madarasa mwengine ili kuweza kuepukana na mlundikano kwa wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.