Habari za Punde

*MSANII MAUA APELEKA MAHABA NIUE NCHINI KENYA

Na Mwandishi wetu, Dar
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya  nchini, Maua Sama ameanza kujitangaza kimataifa baada ya kuanza ziara ya wiki moja nchini Kenya.
Maua ambaye ni zao la THT ataanza kufanya ziara yake leo kwenye ukumbi wa  Privee Westlands ambako atasindikizwa na wasanii nyota wa Kenya kama Dele, Amina, Sege, Heart the Band na wengineo.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Kenya, Maua alisema kuwa ameamua kufanya ziara hiyo ili kujitambulisha  kazika soko la Afrika Mashariki na mipango ipo mbioni kuanza kufanya ziara katika nchi nyingine.
Mbali ya Mahaba Niuwe, Maua pia anatamba na wimbo wake Sisikii pia atafanya mahojiano na vituo mbalimbali vya televisheni, redio na magazeti ya nchi hiyo kwa lengo la kuwapa ufahamu zaidi kuhusiana na muziki wake na vilevile historia.
“Ni faraja sana kufanya ziara  na kutambulisha muziki na kipaji changu cha muziki hapa Kenya, ziara hiyo inalenga kuniongezea mashabaki zaidi nchini Kenya ambako nyimbo zangu  zimekuwa zikifanya vizuri sana,”
“Mashabiki wangu wategemee kupata burudani safi wakati wote wa ziara, hii ni fursa kubwa kwao kuona ‘live’ shoo, lakini pia navishukuru vyombo vya habari Kwa mapokezi mazuri na ushirikiano walionipa mpaka sasa' alisema Maua.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.