Habari za Punde

*NAIBU WAZIRI ANASTAZIA WAMBURA AZINDUA TAMASHA LA TASUBA BAGAMOYO

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo, Anna Wambura (katikati)akifuatilia ngoma ya kikundi cha wanachuo wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) wakicheza ngoma ya Kizaramo ya Mkwaju Ngoma kutoka mkoa wa Pwani.
********************************************************
Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni SAnaa na Michezo, Annastazia Wambura amewataka vijna kutumia fursa ya Tamasha la Kimataifa la 35 la Sanaa na Utmaduni Bagamoyo kuonesha vipaji kwa ajili ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi.

Akifungua Tamasha hilo juzi ambalo mwaka huu limeshirikisha vikundi 65 vya sanaa na utamaduni kutoka nchini na nje ya nchi, Naibu Waziri huyo alisema sanaa ni ajira yenye uhakika kama wasanii watafanya kazi zao kwa uadilifu.

Alisema anafahamu changamoto zinazokikabili chuo cha SAnaa BAgamoyo (TASUBA) za ukosefu wa fedha na wafadhili hivyo aliwataka kushirikisha wadau wa ndani na nje ili matamasha kama hayo yaboreshwe na kushirikisha nchi mbalimbali duniani.

Alisema kutoka TASUBA kianzishwe mwaka 1982 kimekuwa kivutio na kubadilishana tamaduni na nchi mbalimbali kama Ujerumani, Norway, Kenya, Japan na China ambazo zimeshiriki kwaka huu katika tamasha hilo.

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa wizara hiyo, Francis Songoro aliwaomba wadau waendelee kujitokeza kuwatia moyo wasanii katika kazi zao.

Katika tamasha hilo Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo, Anna Wambura aliongoza kucheza ngoma ya kigogo huku kikundi cha wanachuo kikitia fora kwa ngoma ya asili ya Kizaramo kutoka mkoa wa Pwani ya Mkwaju Ngoma.

Awali Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji Majjid Mwanga aliwataka wananchi wa BAgamoyo kukienzi chuo hicho ambacho ni cha kwanza Tanzania kinachozalisha wasanii nchini na kukuza uchumi wa wilaya kwa kuwapokea wageni wengi wanaokuja kujifunza sanaa ya Tanzania.

Tamasha la TASUBA litafanyika kwa wiki mmoja mfululizo ambako vikundi mbalimbali vitaonesha umahiri wao wa kucheza, kuimba na bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa kutumia vifaa vya asili.

Pia katika tamasha hilo ambalo Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) iliwakilishwa na wajumbe sita wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa mtadano huo Suleiman Kissoky ambako kikundi chao cha ngoma na sarakasi cha Splendid kitawakilisha.
Wapiga ngoma wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo (TASUBA) wakipiga ngoma katika ufunguzi wa tamasha hilo. 
Wadau mbalimbali wa sanaa kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia maoneshoa ya ngoma wakati wa ufunguzi juzi. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.