Habari za Punde

*NEC YATOA ELIMU YA MPIGA KURA KWA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA ALAT, MUSOMA


 Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (NEC)  Overblessing Msuya akitoa maelezo kuhusu Mashire ya Kielektroniki ya Usajili wa Mpigakura (BVR)  wananchi waliotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani (wa pili kushoto) akishiriki sala ya kuanza kikao kikao cha pili cha Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) kinachofanyika mjini Musoma mkoani Mara.Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Agsotino Mbogella, Katibu Mkuu wa ALAT Habraham Shamumoyo na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Stephen Mhapa.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara. KWA PICHA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Mchanga Mjaka akifuatilia mada akiwa na wageni waalikwa wenzake kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
 Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Dodoma,  Godwin Kunambi akumuuliza swali  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani kwenye Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
 Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Christina Njovu akimpa maelekezo mwananchi aliyetembelea banda la Tume akiwa na vitambulisho viwili  vya kupigia kura (cha zamani na cha sasa) kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
 Mtoto anayesoma darasa la tano shule ya Msingi Kaminyonge aliyefahamika kwa jina moja la Salvatory (10) akimueleza Mhasibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Hubert Kiata kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu uchaguzi wakati alipotembelea banda la Tume  kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.Katikati na mwandishi wa redio Victoria ya mjini Musoma.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akizungumza na Redio Victoria ya mjini Musoma kuhusu elimu ya mpiga kura.
 Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Aron Msigwa akimsainisha kitabu cha wageni mkazi wa Nyakanga Pius Rigamba wakati alipotembelea banda la Tume kwenye maonesho ya Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika mjini Musoma mkoani Mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa Crispin Luanda akipokea nyaraka mbalimbali kutoka kwa Levina Kakuru  Mtumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni Mtumishi wa Tume, Moshi Makuka. Picha na Hussein Makame-NEC

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.