Habari za Punde

*SERIKALI IMESHALIPA MADAI YOTE YA WALIMU YASIYOKUWA YA MISHARAHARA

Na: Frank Shija, MAELEZO
SERIKALI imewataka walimu wa shule za msingi na sekondari nchini kuwasilisha madai yao yasiyo kuwa ya Mishahara ikiwemo stahili za likizo ili waweze kulipwa madai hayo kwa wakati.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1).

Profesa Ndalichako alisema kuwa Madeni ya Walimu yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni madai yatokanayo na mishahara na yasiyokuwa ya mishahara ambayo yamekuwa yakilipwa na Serikali kupitia Wizara yake ambapo hadi hivi sasa hakuna mtumishi ambaye hajalipwa.

“Hakuna jalada la madai ya walimu yasiyokuwa ya mishahara na kama yapo madai walete ili walipwe kwani fedha zipo”. Alisema Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya mishahara yamekuwa yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo nayo yamekuwa yakifanyika.

Kwa mujibu wa Profesa ndalichako alisema Serikali imekuwa ikipata ufadhili kutoka Serikali ya Sweden kwa ajili ya kusaidia katika kulipa stahili mbalimbali za walimu ili kuboresha weledi wa taaluma yao.

Kwa upande wa ubora wa Elimu, Ndalichako alisema kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika sekta elimu, ubora wa Elimu ya Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia program mbalimbali zikiwemo za mpango wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

Akitolea mfano Waziri Ndalichako alisema kuwa kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi za mpango wa UPE miaka ya 1970 ambao lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kujiunga na elimu ya msingi.

Waziri Ndalichako mwaka 2013 Serikali iliendelea kufanya maboresho kwa kuongeza sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu ili kupata walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo ufaulu wa daraja la tatu kwa wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa masomo mawili katika kidato cha sita.


“Serikali ilianzisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu ya msingi na mafunzo mwanafunzi atatakiwa atasoma darasa la kwanza hadi la 6 kwa msingi na mafunzo ni kuanzia darasa la 7 hadi la 12”.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.