Habari za Punde

*SIMBA YAENDELEA KUJITANUA KILELENI LIGI KUU, YAIRARUA MAJI MAJI MABAO 4-0 TAIFA

Mfungaji wa bao la kwanza na la tatu, wa Simba SC, Jamal Mnyate, akishangilia baada ya kutupia bao la tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar esSalaam, dhidi ya Maji Maji ya Songea. Katika mchezo huo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 yaliyofungwa Jamal Mnyate na Shiza Kichuya. 

MATOKEO MENGINE YA MECHI ZA LEO
Simba 4 - Maji Maji 0
Ndanda Fc 2 - Azam Fc 1
JKT Ruvu 2 - Mbeya City 0
Mtibwa Sugar 1 - Mbao Fc 1
Tanzania Prisons 0 - Mwadui Fc 0
****************************************
TIMU ya Simba leo tena imeendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwararua bila huruma Wanalozombe, Maji Maji kwa mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Kwa ushindi huo Simba SC sasa imefikisha jumla ya pointi 16, baada ya kucheza mechi sita, wakishinda mechi tano na kutoka sare mechi moja. 
Shiza Kichuya akishangilia bao lake la pili...
Kipa Aman Simba akiokoa moja ya hatari langoni kwake dhidi ya Mavugo.
********************************
Bao la kwanza la Simba lilifungwa na hilo, Jamal SImba Mnyate katika dakika ya nne akimalizia mpira uliotemwa na kipa Aman Simba, baada ya shuti kali la Ibrahm Hajib aliyemjaribu kipa wa Majimaji akiunganisha krosi ya Laudit Mavugo.

Hadi Mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0 na kipindi cha pili, Shizza Kichuya, akawainua mashabiki wa Simba kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 67, baada ya beki wa Maji Maji, Lulanga Mapunda kuunawa mpira eneo la hatari.

Alikuwa ni Jamal Mnyate tena aliyepeleka huzuni kwa Wanalizombe hao alipoiandikia Simba bao la tatu katika dakika ya 74 akimalizia krosi ya Mohammed Ibrahim.
Said Ndemla, akimpiga tobo beki wa Maji Maji, Bahati Yusufu.
Kipa wa Maji Maji, Amani Simba akiruka kuokoa moja ya hatari langoni kwake.
********************************
Shiza Kichuya alifunga ukurasa wa mabao katika dakika ya 81, akitupia bao la nne baada ya kufanya kazi kubwa kuambaa na mpira uliopigwa na Nahodha wake Jonas Mkude na kumtoka kipa wa Maji Maji, Amani Simba.

KIKOSI CHA SIMBA
Vicent Agban, Janvier Bukungu, Mohammed Hussein, Juuko Murshid, Jonas MKude ©, Method Mwanjali, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib na Jamal Mnyate

BENCHI LA AKIBA
Peter Manyika, Mohammed Ibrahim, Said Ndemla, Novalty Lufunga, Haji Ugando, Amme Ally na Abdi Banda.

KIKOSI CHA MAJI MAJI
Amani Simba, Bahati Yusufu, Hamad Kibopile, Ernest Raphael, Lulanga Mapunda, Alex Kondo, Luka Kikoti, Enyina Darlington, George Mpole na Paul Mohana.

BENCHI LA AKIBA
Agathon Anthony, Fred Mbuna, Peter Mapunda, Mpoki Mwakinyuke, Marcel Boniventure, Tarik Simba na Hassan Hamis.
Mavugo akijaribu kuwahadaa mabeki wa Maji Maji,....
Hapa ilikuwa ni bonge la Bambi......hadi mtu kapaishwa
Ndemla na Bahati ilikuwa ni patashika....
Ndemla akiwania mpira na Alex Kondo....
Hupiti hapaaa......
Sehemu ya mshabiki wa Simba
Wakishangilia bao..........
Shabiki akipata huduma ya kwanza baada ya kuzimia kwa furaha.....
Mavugo akijaribu kupiga shuti ambalo halikuzaa matunda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.