Habari za Punde

*SIMBA YAKAA KILELENI BAADA YA KUGOMA KULAMBISHWA ICECREAM ZA AZAM FC

 Winga wa Simba SC Shiza Kichuya, akishangilia baada ya kufunga bao pekee katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi yao na Azam Fc uliopigwa kwwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar esSalaam jioni ya leo. Kichuya aliiandikia Simba bao la ushindi katika dakika ya 68 lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo. Hadi mwisho wa mchezo huo Azam Fc 0- Simba Sc 1.

Katika matokeo mengine ya Ligi Kuu leo, Yanga wameendeleza wimbi la ushindi katika mechi zake baada ya kumnyamazisha Kocha mwenye kuchonga Julio kwa kuichapa timu yake mabao 2-0. Mabao hayo yalifungwa na Amis Tambwe katika dakika ya 5 kipindi cha kwanza na Donald Ngoma katika dakika ya 90. Hadi mwisho wa mchezo huo Mwadui Fc 0- Yanga 2.

MATOKEO KAMILI YA MECHI ZA LEO NI:

AZAM FC 0 - SIMBA SC 1
MWADUI FC 0 - YANGA SC 2
MBAO FC 4 - RUVU SHOOTING 0
MTIBWA SUGAR 2 - KAGERA SUGAR 0
MBEYA CITY 0 - TANZANIA PRISONS 0
MAJI MAJI 1 - NDANDA FC 2
 Ilikuwa ni Nginja ngija mguu wa shingo mguu wa roho kati ya mshambuliaji John Bocco na beki Method Mwanjali.
 Bocco akimzidi nguvu Mwanjali.
 Hapa pia ilikuwa ni patashika kati ya Beki Mohamed Hussein 'Tshabalala' na mshambuliaji Ya Thomas Renardo.
 Beki Manjali akiokoa mbele ya Bocco
 Kiungo Salum Aboubakar akipiga pasi ya mwisho.
Lufunga akiwania mpira na Bocco
Beki Shomari Kapombe  akimtoka Mkude.....
Sehemu ya mashabiki wa Azam Fc
 Tshabalala na Ya Thomas........
 Tshabalala akimdhibiti Ya Thomas......
 Ajib Akijaribu kuwatoka mabeki wa Azam Fc......
 Ajibu akiwania mpira na Bruce Kangwa.....
 Sehemu ya Mashabiki wa Simba
Afisa Habari wa Simba, Sunday Manara akishangilia baada ua kumalizika kwa mchezo huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.