Habari za Punde

*SIMBA YAWARARUA MAAFANDE WA RUVU SHOOTING, 2-1, YANGA YALAZIMISHWA KURA MING'OKO NANGWANDA, AZAM YAWALAMBISHA ICECREAM WAJELAJELA 1-0

 Wachezaji wa Simba wakimpongeza mwenzao Ibrahim Ajib,baada ya kuisawazishia timu yake dakika chache tu baada ya kutangulia kufungwa na Ruvu Shooting baola kuongoza katika kipindi cha kwanza katika mchezo wa Ligi Ku Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku bao la pili likifungwa na Laudit Mavugo katika kipindi cha pili.

Na huko Mjini Mtwara katika Uwanja wa nagwanda Sijaona leo Yanga wameshindwa kufurukuta mbele ya wauza Ming'oko, Ndanda Fc, katika mchezo uliokuwa mkali baada ya timu hizo kutoka sare ya 0-0 hadi kumalizika kwa dakika 90 za mchezo huo.

Na katika mchezo mwingine huko jijini Mbeya katika Uwanja wa Sokoine, leo Azam Fc wameweza kuvunja mwiko na kuwashangaza Maafande wa Jela Jela Tanzania Prisons kwa kuwatandika bao 1-0.
 Mweinyi Kazi Mtomo,akiambaa na mpira huku akizongwa na mchezaji wa Ruvu Shooting.
 Laudit Mavugo akiwatoka mabeki wa Ruvu Shooting.
Mashabiki wakishangilia mara baada ya timu yao Simba kusawazisha kwa 1-1 
Laudit Mavugo, akipongezwa na wenzake baada ya kutupia bao la pili.
Kikosi cha Ruvu Shooting
Kikosi cha Simba

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.