Habari za Punde

*TANZANIA NA IRAN KUANZISHA WIKI YA UTAMADUNI

 Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (wa tatu kushoto) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman akielezea azma yake ya kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Utamaduni kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 2,2016 wa pili kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai na kushoto ni Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Iran Bw. Ali Bagiri. 
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa  Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman (katikati) walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2,2016 kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea zawadi ya kiutamaduni kutoka kwa  Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran (katikati) Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman walipokutana Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Serikali ya Tanzania na Iran Septemba 2, 2016 wa kushoto ni Balozi wa Iran nchini Mhe. Mahdi Aga Jafai.
*************************************************
Na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Serikali ya Tanzania na Iran zakubaliana kuanzishwa kwa wiki ya Utamaduni itakayowezesha kujifunza namna ya kuukuza ,kuulinda na kuendeleza sekta hiyo.
Makubaliano hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Iran  Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran.
Waziri Nnauye alisema kuwa amekubaliana na wazo la kuanzishwa  kwa wiki ya Utamaduni kati ya Tanzania na Iran  ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwao namna ya kuukuza, kuulinda na kuuendeleza utamaduni wa mtanzania.

“Utamaduni ni silaha ya upendo na nimefurahia wazo la kuanzisha wiki ya Utamaduni na tuko tayari kujifunza kutoka kwenu na hakika tumelipokea na tunaamini fursa hii italeta mafanikio makubwa katika sekta hii”, alisema Mhe. Nnauye.
Kwa upande wa Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Abuzar Ebrahimi Turkaman aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa wataendelea kushirikiana katika masuala ya Utamaduni na kuendelea kujifunza kutoka kwa watanzania namna bora ya kuuenzi,kuuendeleza na kuutunza Utamaduni.

Naibu Waziri huyo wa Iran aliendelea kusema serikali yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika uandaaji wa Filamu na kubadilishana uzoefu katika masuala ya filamu kati ya nchi hizo mbili.
Hata hivyo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nnauye alipata mwaliko kutoka kwa  Naibu Waziri wa Utamaduni Iran Mhe. Turkaman kwenda nchini Iran kujionea vivutio vya Utamaduni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.