Habari za Punde

TFF WASUSIA MECHI YA WATANI WA JADI, SELCOM WAHAHA KIVYAO KUUZA TIKETI CHEKI HAPA VIDEO

 Meneja Ukuzaji Biashara na Masoko wa kampuni ya Selcom, Juma Mgori (kulia) akiwa na baadhi ya warembo wa kampuni hiyo waliofika Ofisi za Shirikisho la Soka TFF kwa ajili ya kutoa huduma ya kugawa kadi za Smat Card na kuuza Tiketi za kuingilia mchezo wa Watani wa Jadi Yanga na SImba unaopigwa kesho kwwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hekaheka hizo na kutokea sintofahamu kwa baadhi ya mashabiki wa soka nchini kuhusu upatikanaji wa tiketi hizo, inaonekana Shirikisho hilo kususia mchezo huo na kuwaachia zaidi Serikali ambao wameingilia kati kusimamia mapato na kuwaidhinisha Kampuni ya Selcom kusambaza kadi hizo za kutumia Kieletroniki kuingia uwanjani.

Hadi sasa baadhi ya wanahabari na wafanyakazi wa TFF bado hawajajua hatima yao jinsi ya kuingia uwanjani kesho kutekeleza majukumu yao ya kazi kutokana na wahusika kurushiana mpira kuhusu jambo hilo kuwa ni nani anahusika na utoaji wa Kadi za magari ya vyombo vya habari na vitambulisho.
 Baadhi ya mashabiki wakiwa katika foleni ya kupata huduma ya kupatiwa kadi na tiketi nje ya Ofisi za TFF leo mchana.
 Wahudumu wa Selcom wakitoa huduma kwa wateja wao ndani ya uzio wa TFF
 Baadhi ya raia wakiwa nje ya ofisi za TFF....
 Foleni ya kuingia TFF kununua Tiketi
Foleni

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.