Habari za Punde

*TFS YASAIDIA MADAWATI 12,000 MKOANI MWANZA

 Naibu  Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Eng.  Ramo Makani (kushoto)  akimkabidhi  madawati  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ( kulia) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000,  wa  pili kushoto  ni Mtendaji Mkuu wa  Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii 
 Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa  jana  na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela  ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000     
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika Mkoani Mwanzan jana  na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani  kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongela  ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe . 
***************************
Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imekabidhi madawati 12,115 mkoani Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000.

Makabidhiano hayo baina ya TFS na Serikali yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.

Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo , Ramo Makani alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kuhakikisha unakamilisha kutengenenza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya novemba mwezi huu

‘’ Pamoja na kufikia asilimia 61 ya lengo, nawaomba TFS muhakikishe idadi iliyobaki ya madawati inakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao’’ Alisema Makani.
Akizungumza kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo bila kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100 ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na kuwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa taratibu za uvunaji mbao katika baadhi  ya misitu.

TFS tumetekeleza agizo hili kwa kulenga ngazi za chini kabisa za mfumo wa utendaji wa Wakala  ambao ni wilaya. Hivyo katika kugawa idadi ya utengenezaji madawati wa kanda ilizingatia idadi ya wilaya kwa kila kanda’’ alisema Prof. Silayo.

Waziri Makani alisema madawati hayo yatagawiwa katika mikoa ya Simiyu., Kagera, Mara,Geita na Mwanza ambayo itapokea madwati 2,580 yaliyokwisha tengenezwa.


Akizungumz kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela aliwapongeza TFS na kuahidi kuyatunza madwati hayo ili yatumike kwa muda mrefu kwa manufaa ya wanafunzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.