Habari za Punde

*WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA MISAADA YA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

 Waziri Mkuu.Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 5 kutoka kwa  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Shyrose Bhanji ukiwa ni mchango wa mbunge uyo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.Kulia ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles kaijage.
 Waziri Mkuu.Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 37 kutoka kwa group la CEO Roundtable lililowakilishwa na Bi.Santina Benson (wa pili kushoto) ambapo group hilo wamekabidhi mchango huo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea msaada wa mabati yenye thamani ya shilingi milioni 10 kutoka kwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Global Publisher Bw.Erc Shigongo ikiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
 Waziri Mkuu.Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 20 kutoka kwa mwakilishi wa shirika la Trans Ocean Supplies Bi.Melisa Katalaia(wa pili kushoto) ikiwa ni msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles kaijage na wa kwanza kushoto ni katibu mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu Dkt Hamis Mwinyimvua.
Waziri Mkuu.Kassim Majaliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 404 na laki nane kutoka kwa umoja wafanyabiashara wa mafuta Tanzania ukiwa ni mchango wa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.