Habari za Punde

*WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO YAKUTANA NA WAJUMBE KUTOKA WADIGLA MISRI

 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu akifafanua jambo wakati wa  kikao na   wajumbe kutoka WADIGLA Misri (hawapo katika picha), katika kujadiliana masuala mbalimbali na namna  ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta zilizo chini ya wizara.
Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy akieleza jambo wakati wa kikao na wajumbe kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kilichokuwa kikijadili masuala mbalimbali ya namna  ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta ya Michezo, leo Jijini Dar es Salaam,kulia ni Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Kampuni ya Montange Bibi. Teddy Mapunda
Wajumbe ambao ni wakuu wa Idara za kisekta kutoka Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea wakati wa kikao na wajumbe kutoka WADIGLA Misri ambapo walijadili masuala mbalimbali ya namna ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge(katikati) akionyesha mchoro  wa mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru kwa  Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy leo Jijini Dar es Salaam,kushoto ni  Mkurugenzi Mkuu wa WADIDEGLA upande wa Afrika Bw.Rami Nashed.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Joyce Hagu (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo ya mchoro wa mradi wa kituo cha utamaduni kwa Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy leo Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Petro Lyatuu (kulia)akieleza jambo kwa Rais na Mwanzilishi wa WADIDEGLA kutoka Misri Bw. Adel Samy (kushoto), baada ya kikao kilichojadili masuala mbalimbali ya namna  ya kuwezesha ushirikiano wa kuendeleza sekta zilizo chini ya wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo pamoja na wajumbe kutoka WADIGLA Misri wakifuatilia kwa makini fursa video iliyokuwa ikionyesha fursa mbalimbali zinazotolewa na  WADIDEGLA Misri ikiwemo fursa katika sekta ya Michezo yenye lengo la kukuza na kuendeleza michezo mbalimbali. Picha na Lorietha Laurence-WHUSM.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.