Habari za Punde

*YANGA YAPOTEZA MCHEZO WA KWANZA KWA WAPIGA DEBE SHINYANGA STAND UTD 1-0

Na Ripota Wetu Shinyanga
Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, imepoteza mchezo wake wa kwanza tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ambapo haijapoteza katika michezo zake zilizopita na kukubari kupoteza leo katika Uwanja wa Kambarage mbele ya wenyeji wapiga debe Stand United kwa bao 1-0.

Mchezo wa leo uliokuwa wa kukamiana na wenye kasi kwa pande zote mbili ulikuwa na matukio kadhaa ya vurugu na rafu za hapana pale na hadi timu hizo zinakwenda mapumziki zilikuwa sare ya 0-0. Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Pastory Athanas katika dakika ya 58.

Kwa ushindi huo sasa Stand United inapanda hadi nafasi ya pili ikifikisha jumla ya pointi 12,wakiwa nyuma ya Vinara Simba yenye pointi 16, huku Yanga wakibaki Pointi zake 10.

Baada ya mchezo wa leo sasa Yanga wanaingia kambini mjini Pemba kwa ajili ya kuanza kambi ya kujiwinda na Mahasimu wao Simba katika mchezo utakaowakutanisha Oktoba 1 mwaka huu.

Katika dakika ya 62 Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa kiungo Deus Kaseke na kuingia Juma Mahadhi na dakika ya 77 walimtoa Donald Ngoma na kuingia Obrey Chirwa, mabadiliko ambayo hayakuzaa matundahadi kumalizika kwa dakika 90za mchezo huo.

KIKOSI CHA STAND UNITED:
Frank Mwamongo, Revocatus Richard, Adeyum Ahmed, Erick Mulilo, Ibrahim Job, Jacob Masawe, Pastor Athanas, Geremy Katura, Kelvin Sabato, Suleiman Kassim ‘Selembe’ na Adam Kingwande/Abasarim Chidiebere dk86.

KIKOSI CHA YANGA SC: 
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji/Haruna Niyonzima dk86, Vincent Bossou, Andrew Vincent, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Obrey Chirwa dk77, Amissi Tambwe na Deus Kaseke/Juma Mahadhi dk 62.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.