Habari za Punde

*ZANTEL YAKABIDHI ZAWADI YA PROMOSHENI YAKE YA 'JIBWAGE NA MBUZI'

 Kampuni ya simu za mkononi ya ZANTEL jana ilifikia kilele cha Promosheni yake ya Jibwage na mbuzi, ambapo iliweza kukabidhi zawadi kwa wateja wao ambao ni washindi katika Promosheni hiyo.

Wateja walioibuka kidedea katika Promosheni hiyo ya 'JIBWAGE na MBUZI' walikabidhiwa zawadidi zao ambazo ni jumla ya Mbuzi  400 ambapo pia Kampuni hiyo ilikabidhi jumla ya Mbuzi 100 katika vituo mbali mbali vya watoto Yatima nchini.
 Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa Baucha (wa pili kulia) akikabidhi mbuzi kwa washindi wa promosheni ya jibwage na mbuzi. Kulia ni Abdalla Yussuf (wa pili kushoto) ni Arafa Mohamed Dadi na Abrahman Mohamed Abdalla (kushoto).

 Meneja mauzo wa Zanztel, Yussuf Ismail (kulia) akikabidhi mbuzi wa mshindi, Hemed Ali Omar jana.
Mbuzi wanaosubiri kuchukuliwa na washindi wa promosheni ya jibwage na mbuzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.