Habari za Punde

AZAM FC WAIBUKIA KAGERA NA KUWASHUSHA STAND UNITED

Mabao ya Mudathir Yahya, Frank Domayo na John Bocco yameiwezesha Azam Fc kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba dhidi ya Kagera Suga katika mchezo uliomalizika jioni hii.

Katika mchezo huoKagera ndiyi walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 33 kupitia Temy Felix akimalizika mpira wa Krosi iliyopigwa kutoka upande wa kulia.

Dakika saba baadaye Kagera walisawazisha bao hilo kupitia kwa Mudathi Yahya akimalizia mpira wa kichwa uliotengwa na John Bocco.

Hadi mapumziko timu hizo zilitoka uwanjani zikiwa sare ya 1-1, katika dakika ya 80 Kagera walipata penati baada ya beki wa Azam Fc Agrey Morris kuunawa mpira ndani ya eneola hatari, na alikuwa ni Temy Felix tena aliyepiga penati hiyo na kuandika bao la pili kwa Kagera.

Dakika ya 81 alikuwa ni Frank Domayo aliyetokea benchi akiachia shuti kali la nje ya 18 na kuandika baola kusawazisha kabla ya John Boccokushindilia msumari wa mwisho katika dakika ya 84 akiunganisha mpira wa kichwa.

NAFASI NANE ZA JUU LIGI KUU BARA 2016
Simba SC 29
Yanga SC 24
Azam Fc 22
Stand United 21
Kagera Sugar 18
Mtibwa Sugar 17
Tanzania Prisons 15
Ruvu Shooting 15

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.