Habari za Punde

BALOZI IDDI AKUTANA NA RAIS WA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA UWEKEZAJI YA KOYO YA NCHINI JAPAN

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif AliIddi akisalimiana na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya 
Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Norio Shoji Nyumbani kwake Bara bara 
ya Haile Selassie Jijijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyokutoka Japan ukiongozwa na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji 
ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Norio Shoji wa Pili kutoka Kulia 
ukibadilishana mawazo na Balozi Seif. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Bwana Norio Shoji akimueleza Balozi Seif shauku yaKampuni yake kutaka kuwekeza vitega Uchumi Nchini Tanzania kulingana 
na mazingira na rasilmali zilizopo.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Norio aliyepo kati kati mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika nyumbani kwake Bara bara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam. Wa kwanza (Kulia) ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kutoka Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji. Picha na – OMPR – ZNZ.
*******************************************
Kasi kubwa ya uchumi wa Tanzania inayoonekana kupanda kwa haraka
katika kipindi kifupi imeanza kutoa ushawishi mkubwa kwa Makampuni na
Taasisi za Kimataifa kuonyesha dalili za kutaka kuwekeza miradi yao
ya Kiuchumi na maendeleo ili kuunga mkono kasi hiyo.

Rais wa Kamuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo kutoka
Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi Kawaji akiuongoza Ujumbe wa Viongozi
Sita wa Kampuni hiyo alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani kwake Bara
ara ya Haile Selassie Jijini Dar es salaam.

Bwana Koichi Kawaji alisema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na
Wataalamu wa masuala ya Uchumi Duniani umebaini kwamba kasi ya
uchumi wa Taifa la Tanzania unaongoza ikilinganishwa na Mataifa
yaliyomo ndani ya Bara la Afrika kwa hivi sasa .

Kiongozi huyo wa Kampuni ya Kimataifa ya Koto alifahamisha kwamba
Tanzania ni nchi ya kwanza Barani Afrika yenye muelekeo mpana wa
Uchumi wake kukuwa kwa haraka ukifananishwa na Nchi ya Singapore
Bwana Koichi alisema wataalamu wa Kampuni ya Koyo wamelazimika
kufanya ziara ya makusudi katika azma ya kujionea kasi hiyo Nchini
Tanzania na kuangalia maeneo ambayo Taasisi hiyo ya Uwekezaji inaweza
kutumia fursa zilizopo katika kusaidia ukuaji wa Uchumi wa Tanzania.

Alieleza kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilmali za kutosha za
Kiuchumi ambazo kwa namna nyingi Wawekezaji wa ndani na nje ya Nchini
wanaweza kutumiwa vyema katika njia ya kuingia ubia na Serikali,
Makampuni au hata Watu binafsi wenye sifa na shauku ya kuwekeza.

Rais huyo wa Kamuni ya Kimataifa ya Uwekezaji Vitega Uchumi ya Koyo
kutoka Tokyo Nchini Japan Bwana Koichi alielezea furaha yake kutokana
na utulivu mkubwa na Amani iliyotanda Nchini Tanzania katika kipindi
kirefu sasa.

Alisema amani na utulivu huo kwa kiasi kikubwa ndio iliyozaa mafanikio
makubwa ya Uchumi yanayoendelea kupatikana na hatimae kuchangia
mapato ya Taifa sambamba na kupunguza umasikini lakini kwa njia
nyengine pia umezuia mfumko wa bei unaotoa afueni ya maisha bora kwa
Wananchi walio wengi.

Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
ameishauri Serikali ya Japani kupitia ujumbe wa Kampuni hiyo ya Koyo
kuangalia maeneo ambayo Taasisi na Makamuni ya Nchi hiyo yanaweka
kuwekeza.

Balozi Seif alisema Tanzania imepakana na Bahari kuu eneo ambalo Japan
kutokana na kuendelea Kiviwanda inaweza kusaidia Taa luma katika
Mpango wa kulielekeza Taifa la Tanzania kuwa Nchi ya Viwanda ifikapo
Mwaka 2025.

Alisema Tanzania bado ina fursa nzuri ya kujifunza Taaluma ya Uvuvi wa
Bahari kuu kwa kuanzishwa Viwanda vya usindikaji bidhaa zinazotoka na
mazao ya Baharini kama Samaki wa aina mbali mbali pamoja na zao la
Mwani.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuhakikishia Uongozi wa Kampuni
hiyo ya Kimataifa ya Uwekezaji ya Koyo kwamba Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibat itakuwa tayari kutoa msaada wowote utakaohitajiwa na Kampuni
hiyo wakati itakapofikia hatua ya kutaka kuwekeza miradi yake
Visiwani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.