Habari za Punde

BILL- THE MEDIA SERVICES ACT 2016Sheria ya Huduma za Habari
39
Mamlaka yanidhamu
17.
-(1) Bodi itakuwa na mamlaka ya nidhamu, na Waziri atakuwamamlaka ya mwisho ya rufaa kuhusiana na Mkurugenzi Mkuu naWakurugenzi wengine.(2) Mkurugenzi Mkuu atakuwa mamlaka ya nidhamu na Bodi itakuwamamlaka ya mwisho ya rufaa kuhusiana na wafanyakazi wa Bodi.
(c) Uthibitishwaji wa Wanahabari
Ithibati yaWanahabari
18.-
(1) Mtu hataruhusiwa kufanya kazi za uandishi wa habari,isipokuwa kama mtu huyo amethibitishwa na Sheria hii.(2) Mtu ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi wa habariataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi utakaoainishwakatika kanuni.(3) Mwanahabari ambaye si raia wa Jamhuri ya Muungano auasiyetambuliwa kama mkazi wa kudumu kwa mujibu wa Sheria za Uhamiajianaweza kuthibitishwa kwa sababu maalum kwa muda usiozidi siku sitini.(4) Pale ambapo kipindi cha uthibitisho kilichotolewa chini ya kifungukidogo cha (3) kimeisha muda wake na madhumuni ya uthibitisho husikahayajakamilika, mwanahabari husika anaweza kuomba kwa Bodi kuongezewamuda usiyozidi siku ishirini na moja.(5) Bodi inaweza kufuta uthibitisho wa mwanahabari ikiwaitajiridhisha kwamba-(a)
mwanahabari amekiuka kwa kiasi kikubwa maadili ya taalumayaliyoainishwa katika kanuni za maadili ya taaluma ya habari; au(b)
ikiwa mwanahabari si raia wa Tanzania, mwanahabari huyohatekelezi lengo la uthibitisho wake.
Kitambulishochamwanahabari
19.-
(1) Mwanahabari aliyethibitishwa kwa mujibu wa Sheria hiiatapewa kitambulisho na Bodi.(2) Kitambulisho kitakuwa ni uthibitisho kuwa mmiliki nimwanahabari aliyethibitishwa, na muda wa kitambulisho utakuwa kamaitakavyoainishwa katika kanuni.(3) Mmiliki wa kitambulisho anaweza, baada ya kuisha muda wakutumika wa kitambulisha na kulipa ada iliyoainishwa, atatuma maombi yakupewa upya kitambulisho.
Orodha yaWanahabari
20.-
(1) Bodi itatunza Orodha ya Wanahabari itakayojumuisha majinana maelezo ya wanahabari waliopo waliothibitishwa.(2) Mtu aliyekoma kuwa mwanahabari kutokana na kuondolewa jinalake kwenye Orodha ya Wanahabari au kusimamishwa kufanya kazi yauandishi wa habari hataruhusiwa kufanya kazi ya uandishi wa habari kwanamna yoyote ile.(3) Mwanahabari aliyethibitishwa ambaye jina lake limeondolewakwenye Orodha ya Wanahabari au amesimamishwa hataruhusiwa kuajiriwa aukushughulika kwa namna yoyote ile katika kazi au taaluma inayohusiana nahabari.

Sheria ya Huduma za Habari
40
(4) Bila kujali masharti ya kifungu kidogo cha (2) na (3), endapo jinala mwanahabari limeondolewa kwenye orodha ya wanahabari au uthibitishowa mwanahabari yeyote umesimamishwa kwa mujibu wa kifungu hiki, Bodiinaweza, kwa uamuzi wake au kwa maombi ya mwanahabari husika kupitiautarartibu utakaowekwa, na katika hali yoyote ile, baada ya kufanya uchunguzikwa kadri Bodi itakavyoona inafaa, itaelekeza kwamba-(a)
kuondolewa kwenye Orodha kumethibitishwa;(b)
 jina la mwanahabari huyo lirudishwe kwenye Orodha; au(c)
kusimamishwa kwa mwanahabari aliyethibitishwa kuondolewe.(5) Bodi itatangaza Orodha ya Wanahabari katika
Gazeti
 la Serikali augazeti ambalo linasomwa na watu wengi.
(d) Mfuko wa Mafunzo wa Habari
Kuundwa kwaMfuko
21.-
(1) Kunaundwa Mfuko utakaojulikana kama Mfuko wa Mafunzoya Habari utakaosimamiwa na Bodi.(2) Malengo ya Mfuko yatakuwa ni-(a)
kuwezesha mafunzo kwa wanataaluma ya habari;(b)
kukuza programu za uendelezaji maudhui ya ndani ya nchi; na(c)
kukuza na kuchangia utafiti na maendeleo katika nyanja za habarina mawasiliano ya umma.
Vyanzo vyafedha za mfuko
22.
Vyanzo vya Fedha za Mfuko vitatokana na-(a)
fedha itakayoidhinishwa na Bunge;(b)
misaada, zawadi na michango;(c)
michango ya hiari kutoka kwenye vyombo vya habari; au(d)
fedha ambayo kwa namna yoyote italipwa au kuwekwa kwenyeMfuko kwa masharti ya Sheria hii, au kuhusiana na auzinazoendana na utetekelezaji wa majukumu chini ya Sheria hii.SEHEMU YA NNEBARAZA HURU LA HABARI
Uanzishaji waBaraza
23.
 Linaanzishwa Baraza litakalofahamika kama Baraza Huru laHabari.
Uanachama nauendeshaji waBaraza
24.
-(1) Kila mwanahabari aliyethibitishwa atakuwa mwanachama waBaraza.(2) Waziri, kwa Tangazo litakalotolewa katika
Gazeti
 la Serikaliataitisha mkutano wa kwanza wa Baraza kwa madhumuni ya kuchaguaviongozi wa Baraza.(3) Viongozi wa Baraza watajumuisha-(a)
Mwenyekiti wa Baraza;(b)
Makamu Mwenyekiti wa Baraza; na(c)
wanahabari wengine wawili watakaopendekezwa na taasisi zahabari.

Sheria ya Huduma za Habari
41
Kazi za Baraza
25.
-(1) Kazi za Baraza zitakuwa-(a)
kwa kushirikiana na Bodi:
(i)
kuandaa na kuidhinisha kanuni za maadili ya taaluma yawanahabari;
(ii)
kukuza maadili na viwango vya taaluma baina yawanahabari na kampuni za habari;(b)
kufanya marejeo juu ya utendaji wa sekta ya habari;(c)
kushirikiana na wadau katika kukuza wajibu wa vyombo vyahabari; na(d)
kufanya kazi nyingine za uhamasishaji kama Baraza, kwa azimiolitakavyoamua;(2) Baraza katika kutekeleza kazi zake itazingatia umoja wa kitaifa,usalama, uhuru wa nchi, uadilifu na maadili na maadili ya jamii kwa wajumbewake.
Kamati zaBaraza
26
.-(1) Baraza, kwa madhumuni ya kuwezesha utekelezaji wa kazizake chini ya Sheria hii, litaunda kamati kadhaa kwa ajili utekelezaji wa kazimaalum kama itakavyoamuliwa na Baraza.(2) Kamati zitakazoundwa na Baraza zitajumuisha kamati yamalalamiko itakayoshughulikia malalamiko yanayohusu maudhui yamachapisho.(3) Baraza linaweza, mzingoni mwa mambo mengine, kutengenezakanuni zinazoainisha:(a)
mienendo na taratibu zitakazosimamia malalamiko yanayohusumaudhui ya machapisho; na(b)
tuzo zinazoweza kutolewa na kamati ya malalamiko.
Rufaa
27.
 – 
(1) Isipokuwa kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 38, mtuambaye hakuridhishwa na tuzo iliyotolewa na Baraza, anaweza kukata rufaaMahakama Kuu.(2) Malalamiko hayo yataambatanishwa na nakala ya maudhui yachapisho linalolalamikiwa.(3) Mahakama Kuu, wakati wa kusikiliza rufaa, itapitia lalamikohusika, na kama itakuwa muhimu, kuwaita wahusika katika shauri hilo kutoauthibitisho au utetezi wao.
Mienendo navikao vya Baraza
28.
-(1) Kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii, Baraza-(a)
litaamua idadi ya vikao vitakavyoitishwa mara kwa mara; na(b)
litakuwa na mamlaka ya kutengeneza utaratibu wake kuhusianana vikao au shughuli zake.(2) Baraza, mara kwa mara, litakubaliana juu ya:(a)
muda na mahali pa kufanya vikao vya mwaka vya wadau namasuala mengine yanayohusiana na hayo;(b)
utaratibu wa kusimamia na kugharamia kazi za Baraza;(c)
muundo wa Baraza kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake;na(d)
taratibu au namna ya kutambua na kualika vyama vya habari autaasisi zinazojihusisha na habari.

Sheria ya Huduma za Habari
42
Uteuzi waKatibu waBaraza
29.
-(1) Kutakuwa na Katibu wa Baraza ambaye atateuliwa na Barazakwa kushindanishwa.(2) Katibu atashika madaraka kwa kipindi cha muda wa miaka mitatuna anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine.
Kazi za Katibuwa Baraza
30.
 Katibu wa Baraza atakayeteuliwa kwa mujibu wa Sheria hiiatakuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza na atawajibika-(a)
kutekeleza majukumu ya kila siku ya Baraza;(b)
kuhakikisha kuwa fedha za Baraza zinatumika ipasavyo,kutolewa taarifa za hesabu na kutumika kwa madhumuni husika;(c)
kutunza kumbukumbu za shughuli za Baraza; na(d)
kutekeleza majukumu mengine kama Baraza litakavyompangia.
Uondolewaji waKatibu
31.
 Bila kujali masharti ya kifungu cha 31, Katibu anawezakuondolewa madarakani na Baraza kwa mujibu wa vigezo na masharti ya kaziikiwa-(a)
amepoteza uwezo wa kutekeleza majukumu yake kutokana nasababu za kimaumbile au ugonjwa wa akili;(b)
ataonyesha tabia au mwenendo usiokubalika;(c)
atakosa uwezo au kushindwa kutekeleza majukumu yake;(d)
atakiuka kanuni; au(e)
kwa sababu nyingine yoyote ambayo itahalalisha kuondolewakazini kwa vigezo na masharti ya kazi.SEHEMU YA TANOKASHFA
Kashfa kwamaneno
32.-
(1) Jambo lolote, kama likichapishwa, kutangazwa linawezakuharibu sifa ya mtu yeyote kwa kumfanya achukiwe, adharauliwe auafanyiwe kejeli au linaloweza kumharibia mtu kazi yake kwa kuchafua jinalake au kumvunjia heshima yake, jambo hilo litahesabika kuwa ni kashfa.(2) Jambo linaloelezwa katika kifungu kidogo cha (1) litakuwa suala lakashfa hata kama limechapishwa au kutangazwa dhidi ya mtu aliyefarikidunia.(3) Mashtaka ya kashfa yanayomhusu mtu aliyefariki dunia hayawezikufunguliwa isipokuwa kwa idhini ya maandishi ya Mkurugenzi wa Mashtaka.
Habari kwa njiaya chapisho
33.-
(1) Mtu atahesabika kuwa amechapisha suala la kashfa, ikiwa mtuhuyo amesababisha kuchapishwa, kuandikwa, kuchorwa, kutengenezwakaragosi au kwa namna nyingine yoyote ambayo suala la kashfalimewasilishwa, limeshughulikiwa, ama kwa maonesho, kusomwa,kunakiliwa, kuelezwa, kupokelewa au vinginevyo, kwa njia ambayo maana yakashfa itajulikana au inaweza kujulikana kwa mtu aliyekashifiwa au mtumwingine yeyote.(2) Haitakuwa lazima kwamba uchapishaji au utangazaji wa kashfaumetolewa kwa waziwazi au kikamilifu.

Sheria ya Huduma za Habari
43
(3) Kwa madhumuni ya kifungu kidogo cha (2), inatosha kama kashfahiyo inaeleweka kuwa inamhusu huyo mtu aliyekashfiwa kutokana na maelezoya kashfa yenyewe au kutokana na mambo mengine yasiyofungamana namaelezo hayo ya kashfa au kutokana na baadhi ya maelezo hayo na ya mambohayo mengine.
Ufanunuzi wautangazaji usiohalali
34.
Utangazaji wa mambo yenye kashfa utahesabika kuwa si halalikwa madhumuni ya Sehemu hii ya Sheria hii, isipokuwa kama-(a)
mambo yenyewe ni ya kweli na yanatangazwa kwa manufaa yaumma; na(b)
umeruhusiwa kama mojawapo ya sababu zilizoainishwa ndani yaSheria hii.
Utangazaji wamambo yenyekashfa ambayoni halali
35.-
(1) Utangazaji wa mambo yenye kashfa utaruhusiwa na hapanamtu yeyote anayeweza kuadhibiwa kwa sababu hiyo, ikiwa-(a)
mambo hayo yanatangazwa na Rais, Serikali au Bunge katika hatiyoyote ya Serikali au shauri la mashtaka;(b)
mambo hayo yanatangazwa katika Bunge na Rais, Serikali,Mbunge au Spika;(c)
mambo hayo yanatangazwa kwa amri ya Rais au Serikali;(d)
mambo hayo yanatangazwa kuhusu mtu yeyote ambayeanatakiwa kufuata sheria na kanuni za jeshi au jeshi la wanamajina yametangazwa kuhusu tabia yake kama mtu wa kazi hizo namtu aliye na mamlaka juu yake kuhusu tabia hiyo;(e)
mambo hayo yanatangazwa wakati wa kusikilizwa kwa shaurilolote mahakamani na yanatangazwa na mtu anayeshiriki katikashauri hilo kama Jaji, hakimu, kamishna, wakili, mzee wa baraza,shaidi au muhusika katika shauri hilo;(f)
mambo hayo yanayotangazwa ni taarifa ya kweli na sahihi ya jambo lolote lililosemwa, lililotendwa au lililotangazwa katikaBunge; au(g)
mtu huyo anayetangaza mambo hayo anapaswa, kwa mujibu washeria, kutangaza mambo hayo.(2) Pale ambapo utangazaji wa mambo yenye kashfa umeruhusiwa, basi kwa madhumuni ya Sehemu hii ya Sheria hii, si muhimu kama mambohayo ni ya kweli au ya uongo, na kama inajulikana au haijajulikani auinasadikiwa kuwa ni ya uongo na kama yametangazwa ama kwa nia safi au la.(3) Hakuna jambo lolote katika kifungu hiki litakalo msalimisha mtuyeyote na jukumu la kuadhibiwa kwa mujibu wa Sehemu yoyote ya Sheria hiiau sheria nyingine yoyote kwa makosa ya madai au ya jinai, ikiwa utangazajiwa jambo ambalo limeruhusiwa umezuiliwa au nafuu ya mtu aliyeathirikaimetolewa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Utangazaji wamambo yenyekashfa si halaliila kwa MashartiMaalum
36.
Utangazaji wa mambo yenye kashfa utahesabika kuwaumeruhusiwa kwa masharti maalum ikiwa mambo hayo yanatangazwa kwa niasafi na ikiwa uhusiano baina ya mtu anayetangaza na mtu anayetangaziwamambo hayo unamfanya mtu huyo mtangazaji kuwa na jukumu lakumtangazia huyo mtu mwingine ama kwa mujibu wa sheria au kufuatana na

Sheria ya Huduma za Habari
44
mila au kanuni za mwenendo bora katika jamii kwa jumla au ikiwa mtangazajihuyo anatekeleza maslahi yake yaliyo halali kwa kutangaza mambo hayo, kwasharti kwamba katika hali kama hiyo utangazaji huo hauzidi ama kwa ukubwaau kwa namna yake, na pia utangazaji utahesabika kuwa umeruhusiwa kwamasharti maalum kwa mujibu wa masharti yafuatayo, yaani ikiwa-(a)
mambo yanayotangazwa ni taarifa ya kweli na sahihi ya jambololote lililosemwa, lililotendwa au lililoonekana katika shaurilolote la madai au la jinai linalosikilizwa mahakamani; isipokuwakwamba iwapo mahakama itapiga marufuku utangazaji wa jambololote lililosemwa au lililoonekana katika mahakama hiyo kwasababu kwamba jambo hilo huchochea uasi, ni ovu au ni lakukufuru basi utangazaji wa jambo kama hilo hautahesabikakuwa ni halali;(b)
mambo yanayotangazwa yametokana na nakala au muhtasarihalisi wa mambo yaliyopata kutangazwa wakati uliopita, na ikiwautangazaji wa mambo hayo wakati uliopita ulikuwa halali, kwamujibu wa Sehemu hii ya Sheria hii;(c)
mambo hayo ni maoni yaliyotolewa kwa nia safi kuhusu vitendovya kikazi vya mtu yeyote mwenye madaraka katika shughuli zaMahakama, kiofisi au majukumu ya umma, au tabia yake binafsikwa kadri tabia hiyo inavyoonekana katika vitendo vya kikazi;(d)
mambo hayo ni maoni yaliyotolewa kwa nia safi kuhusu vitendovya mtu yeyote vinavyohusika na suala la jambo lolote linalohusuumma, au kuhusu tabia yake binafsi kwa kadri tabia hiyoinavyoonekana katika vitendo kama hivyo;(e)
mambo hayo ni maoni yaliyotolewa kwa nia safi juu ya tabia yamtu yeyote kama ilivyoonekana kwenye ushahidi uliotolewakatika shauri lolote la kisheria lililosikilizwa hadharani, kama nishauri la madai au la jinai kuhusu tabia ya mtu yeyote ambayekatika shauri hilo anashiriki kama mshtaki au mshtakiwa, mdai aumdaiwa, shahidi au anashiriki kwa namna nyingine yoyote, aukuhusu tabia binafsi kwa kadri tabia hiyo inavyoonekana kwa jinsi ilivyoelezwa katika aya hii;(f)
mambo hayo ni maoni yaliyotolewa kwa nia safi kuhusu ubora wakitabu chochote, maandishi, picha au mchoro, hotuba au shughulinyingineyo yoyote, maonesho au tendo lililotangazwa aukutendwa kwa hadhara au lililotendwa au kutolewa hadharanikwa ajili ya kutaka kupata maoni ya watu, au kuhusu tabia binafsiya mtu yoyote anayehusika na lolote kati ya mambo hayoyaliyotajwa kwa kadri tabia hiyo inavyoonekana katika mambohayo;(g)
mambo hayo ni lawama iliyotolewa na mtu kwa nia safi kuhusuvitendo vya mtu mwingine katika jambo lolote ambalo huyoaliyetoa lawama ana mamlaka nalo, ama kwa mujibu wa mkatabaau vinginevyo na kwa kadri anavyohusika huyo aliyelaumiwa aukuhusu tabia binafsi ya mtu huyo aliyalaumiwa kwa kadri tabiahiyo inavyoonekana katika vitendo hivyo;

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.