Habari za Punde

BODI YA MFUKO WA BARABARA YAZUIA MALIPO YA MIRADI YA BARABARA MANISPAA YA KINONDONI

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na maamuzi ya kusitisha utoaji fedha kwa miradi yote iliyo chini ya mfuko huo kutokana na matumizi mabaya ya fedha hizo kwa Manispaa ya Kinondoni. Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule (kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na maamuzi ya kusitisha utoaji fedha kwa miradi yote iliyo chini ya mfuko huo kutokana na matumizi mabaya ya fedha hizo kwa Manispaa ya Kinondoni. Kutoka kushoto ni Eliudi Nyauhenga Kaimu Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini na Injinia Rashid Kalimbaga Naibu Meneja Ufundi, Bodi ya Mfuko wa Barabara.
*********************************************
BODI ya Mfuko wa Barabara imesitisha kutoa fedha na kusimamisha miradi yote ya ujenzi wa barabara zinazogharamiwa na bodi hiyo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa kile kubaini matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na mfuko huo ikiwamo kiwango kibovu cha barabara zinazojengwa katika manispaa hiyo. 

Bodi hiyo imesitisha malipo hayo na kusimamisha miradi hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati ikizungumza na vyombo vya habari kuelezea dosari zilizofanywa na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni. 

Akizungumza Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara, Joseph Haule alisema uamuzi wa bodi umefikiwa baada ya kikao chake cha 67 kilichofanyika mwezi Septemba kupitia taarifa mbalimbali zikiwemo za utendaji. 

Alisema bodi hiyo imesimamisha upelekaji fedha za mfuko wa barabara Manispaa ya Kinondoni baada ya kubaini urasimu mkubwa katika ujenzi wa barabara ya Masjid-Quba ya zaidi ya kilomita mbili (2.478km) iliyopo Sinza Mori na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika manispaa hiyo kujengwa chini ya kiwango jambo ambalo limeitia hasara Serikali. Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na maamuzi ya kusitisha utoaji fedha kwa miradi yote iliyo chini ya mfuko huo kutokana na matumizi mabaya ya fedha hizo kwa Manispaa ya Kinondoni. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, Joseph Haule akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na maamuzi ya kusitisha utoaji fedha kwa miradi yote iliyo chini ya mfuko huo kutokana na matumizi mabaya ya fedha hizo kwa Manispaa ya Kinondoni. Kutoka kushoto ni Eliudi Nyauhenga Kaimu Meneja wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini na Injinia Rashid Kalimbaga Naibu Meneja Ufundi, Bodi ya Mfuko wa Barabara. Baadhi ya maofisa wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na maamuzi ya kusitisha utoaji fedha kwa miradi yote iliyo chini ya mfuko huo kutokana na matumizi mabaya ya fedha hizo kwa Manispaa ya Kinondoni.
********************************
Haule alisema Barabara ya Masjid-Quba licha ya kujengwa chini ya kiwango imekiuka taratibu za manunuzi kwa Mkandarasi ikiwemo mkandarasi kupewa tenda hiyo bila kufanya mazungumzo (negotiations) huku mradi huo ukichelewa kumalizika hadi muda huu. 

Ujenzi ulianza Machi 2015 na ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu lakini hadi muda huu mjenzi haujakamilika na tayari mkandarasi amelipwa kiasi cha zaidi ya milioni 201 zimelipwa kinyume cha taratibu. 

Haule aliongeza kuwa barabara hiyo ambayo hadi sasa imejengwa kwa urefu wa mita 700 tu watendaji wa Manispaa wameshindwa kutoa nyaraka za mikataba kwa wakaguzi jambo ambalo ni kuvunja sheria na kanuni. 

Alisema bodi pia imebaini mapungufu katika miradi mingine ikiwemo; ujenzi wa barabara ya Mabatini Police kwa kiwango cha lami, ujenzi wa barabara Akachube, ujenzi wa barabara ya Sayansi na barabara ya Biafra France Embassy ambapo zimeharibika muda mfupi baada ya ujenzi hivyo kuitia hasara Serikali. "...Barabara zote zilizotajwa hapo juu zimeharibika mapema kuliko ilivyotarajiwa na hivyo kuitia hasara Serikali. 

Barabara hizi zimekuwa na mashimo na ni kero kwa watumiaji wa barabara ambao ndio wanaolipa tozo za barabara," alisema Mwenyekiti huyo wa Mfuko wa Barabara. 

Alisema Manispaa ya Kinondoni imekuwa na tabia za kutumia fedha za mfuko wa barabara kwa kazi ambazo hazipo katika mpango kazi uliokubaliwa, mfano ni matumizi ya fedha bilioni moja kujenga barabara za Chwaku na Migombani kwa vipande vya zege tena chini ya kiwango, badala kutumia kiasi hicho kuziba mashimo kwenye barabara zake zilizoharibiwa na mvua mwaka 2014/15. 

"Bodi imeamua kusimamisha mara moja kazi zote zinazogharamiwa na mfuko wa barabara zinazosimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni hadi hapo mifumo thabiti ya usimamizi wa fedha za mfuko wa barabara itakapowekwa...," alisema Haule. 

Pamoja na hayo amemuomba Katibu Mkuu TAMISEMI kuchukua hatua kwa maofisa wote waliohusika kwa mapungufu yote yaliyoonekana katika miradi ya barabara ukiwemo wa Masjid-Quba na kuhakikisha fedha 354,285,105 zilizotumika ujenzi wa zege chini ya kiwango zinarejeshwa katika akaunti ya Bodi ya Barabara. Mkutano wa maofisa wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ukiendelea.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.