Habari za Punde

YANGA YAPIGA AJWA,YAMREJESHA KOCHA PLUIJM YAGOMEA BARUA YAKE YA KUJIUZULU
Waziri Nchemba (katikati) akizungumza na kocha Pluijm
Waz
iri Nchemba (katikati) akizungumza na kocha Pluijm (kulia) na Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit.

Mh. Nchemba ameingilia kati na kumrejesha kazini kocha wa Yanga Hans Van De Pluijm ambaye aliandika barua ya kujiuzulu hivi karibuni baada ya kuenea tetesi za kuwasili Kocha mpya Mzambia na kuomba kujiuzulu kuiongoza timu hiyo.

Katika mazungumzo yaliyodumu kwa takribani siku tatu, hatimaye Mchana huu Mwigulu Nchemba amefanikiwa kumshawishi na kumrejesha kocha huyo ndani ya viunga vya jangwani na tayari kwa kuendelea na kazi yake ya Ukocha.

Hii ni mara ya pili mwigulu nchemba anafanikiwa kuweka mambo sawa ndani ya Club ya hiyo ya Yanga, ambapo msimu uliopita alifanikiwa kumrejesha Kiungo Haruna Niyonzima kuichezea Yanga baada ya kutokea mtafaruku baina yake na Klabu hiyo.

Aidha Waziri Mwigulu ambaye ni mpenzi na mwanachama wa Yanga, aliushauri uongozi kumrudisha Pluijm na baadaye kuzungumza na kocha huyo pia kumshauri akubali kurejea.

Baadaye aliamua kuzikutanisha pande zote mbili, Pluijm na uongozi wa Yanga katika kikao ambacho inaelezwa makubaliano yalifikiwa.

Nao Yanga tayari wameshamwandikia barua ya kumjibu kocha huyo 

kutokukubaliana na ombi lake la kujiuzuru.

Katika barua iliyosainiwa na Katibu, Baraka Deusdedit, Yanga imesema haioni sababu ya kuachana na Mholanzi huyo baada ya mafanikio aliyoipa klabu.

Mholanzi huyo alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina bila kumtaarifu, ambapo kocha huyo aliamua kuondoka na kukutaa nafasi aliyokuwa ametangaziwa ya Ukurugenzi wa Benchi la ufundi.

Baada ya mazungumzo hayo leo uongozi wa Yanga umemuandikia barua Pluijm kumuomba rudi kazini kuelekea maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao siku ya jumapili.Uongozi wa Yanga ulitaka kumuondoa Pluijm na Wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh wote wazalendo na kuwaleta Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua. 


WASIFU: alizaliwa  mwaka 1949, alianza kuifundisha Yanga mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts.


Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana. 

Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm aliondoka baada ya kutofautiana na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.

Pluijm alitaka kuondoka Jangwani baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 124, akishinda 77, sare 25 na kufungwa 22.

Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 106 za tangu mwaka jana, alisema 66, sare 19 na kufungwa 20.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.