Habari za Punde

CCBRT YATOA MAFUNZO MAALUM KWA MATUMIZI YA VIFAA VYA KUIMARISHA HUDUMA KWA WATOTO WACHANGA

Mchomvu kutoka CCBRT akitoa mafunzo kwa Madaktari walioshiriki katika mafunzo ya kutumia Vifaa hivyo ili kufanya zoezi hilo kwa ufanisi liweze kuleta matokeo mazuri
Muuguzi msaidizi wa watoto katika hospitali ya Muhimbili Bi Miriam ambaye pia ni miongoni mwa wanafunzi wanaonufaika na mafunzo hayo akifurahi jambo wakati wa mafunzo hayo yakiendelea.Bi Miriam alisema mafunzo hayo yatawaongezea ufanisi mkubwa katika utendaji wa kazi
Mkufunzi mkuu wa mafunzo hayo Daktari Yaser Abdallah amesisitiza umuhima wa elimu Zaidi kutolewa kwa wauguzi na kusisitiza kwamba mafunzo hayo yatolewe kwa kiwango cha juu Zaidi Anaiomba serikali ya Tanzani pamoka na wadau wengine kuunga mkono kujitahidi zinazofanywa na CCBRT kutoa misaada Zaidi na kushiriki kwa pamoja kuboresha huduma ya afya katika hospitali zote na sio tu hospital za rufaa.
**********************************
Kupitia mpango wa kutoa mafunzo ya Uzazi na vichanga (Maternal & Newborn) unaofanya kazi kwa wasaidizi wa Afya kutoka kwenye vituo 23 katika mkoa wa Dar Es Salaam. 
CCBRT kwa kuendeleza jitihada zake za kuhakikisha inapunguza idadi ya vifo vya watoto wachanga na wanaozaliwa kabla ya muda imeanza rasmi kutoa mafunzo maalum ya jinsi ya kutumia vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha huduma kwa watoto wachanga. 

Mpango huu umewezeshwa na Vodacom Foundation na mafunzo haya maalum yatasaidia wauguzi ili kuweza kuvitumia Vifaa hivyo kwa ufanisi Zaidi katika jitihada za kupunguza vifo vya watoto wachanga, watoto wanaozaliwa kabla ya muda (pre maturity), watoto wanaozaliwa na maambukizi na wale wanaozaliwa na tatizo la mfumo wa hewa. Lengo kuu ni kushiriki katika harakati za kupunguza vifo vya watoto wachanga katika mkoa wa Dar es Salaam.
Wataalam wa kiufundi waliotengeneza vifaa hivyo nao wamefika nchini kutoa mafunzo kwa madaktari wa watoto wachanga kuhusu jinsi ya kuvitumia na kuvitunza vifaa hivyo, pia kwa makampuni ya Kitanzania kwa ajili ya urekebishaji kama vikipata hitilafu. 
Mafunzo hayo ambayo yatatolewa kwa muda wa wiki moja katika hospital kuu ya Rufaa Muhimbili yamejumuisha wauguzi wa watoto wachanga kutoka hospital kuu za rufaa mkoani Dar es salaam ambazo ni Temeke Amana ,Mbagala na Mwananyamala

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.