Habari za Punde

CHIDIEBELE WA STAND UNITED AVUNJIKA TAYA, KUPUMZIKA WIKI SITA, AZAM WAMTEMTEMBELEA

 Baadhi ya wachezaji wa Azam Fc, wakimpa pole na kupiga picha ya kumbukumbu na mchezaji wa Stand United Chidiebele, aliyeumia na kuvunjika Taya kwa kugongana na beki wa Agrey Morris (kulia kwake) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kati ya Stand na Azam jana. 

Mchezaji huyo aliumia na kukimbizwa Hospitali kwa matibabu na baadaye kugundulika kuwa amevunjika Taya, Hivi sasa amewekewa nyaya mdomono katika meno ili kumsaidia kuunga mishipa ambapo hawezi kuongea kwa sasa na anahudumiwa kwa kupatiwa vyakula laini kama supu ya samaki na dagaa, juisi Fresh Nature kutokana na kwamba hawezi kufungua mdomo hadi baada ya Wiki sita kwa mujibu wa Daktari wake.
 Chidi akiwa Hospitali jana baada ya kuumia
 Chidi akinyweshwa Uji...
Chidi akiwa mapumzikoni

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.