Habari za Punde

HALMASHAURI YA MEATU YATAKIWA KUANDAA MFUMO WA BIASHARA KWA VIJANA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama kulia akicheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokua kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha maziwa Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu. Kushoto ni Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus Kamani.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (wapili kushoto) akiangalia moja ya jiko la kuandalia maziwa kabla ya kuyasindika alipotembalea kiwanda hicho wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiangalia moja ya kifungashio cha maziwa ambacho tayari kimeshawekewa maziwa wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico
 : Baadhi ya vijana wa Meatu Milk akimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Rachel Kasanda akizungumza na vijana wa Meatu Milk (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (kulia) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus Kamani.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (aliyesimama) akizungumza na vijana wa Meatu Milk (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dkt. Titus Kamani.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akimpa zawadi ya gudulia la maziwa yanayotengenezwa na Vijana wa Meatu Milk Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (kulia)  wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto aliyesimama) akipokea mchango wa kuchangia uendelezaji wa Meatu Milk kutoka kwa Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Mkurugenzi wa Meatu Bw. Fabian Manoza Said (kulia) zaidi ya shilingi milioni nne zilizokusanywa wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk kuendeleza kiwanda hicho jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule ya sekondari Meatu wakifuatilia matukio yaliyokua yakiendelea wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Wananchi wa Meatu wakimsikiliza mageni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Meatu Milk jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.

Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM, Simiyu
*************************************************
Na: Genofeva Matemu – WHUSM, Simiyu
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu imeombwa kuwatengenezea mfumo wa kibiashara vijana wa Meatu Milk ili waweze kuboresha na kuendeleza bidhaa ya maziwa yanayotengenezwa na kiwanda hicho.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama alipotembelea kiwanda Meatu Milk na kufungua jiwe la uzinduzi wa mradi wa kusindika maziwa jana katika Halmashauri ya Meatu Mkoani Simiyu.
Mhe. Jenista amesema kuwa mradi wa usindikaji maziwa ni mradi utakaowavuta wafugaji wengi kuondokana na tatizo la kuangaika na mifugo yao kwa sababu soko la maziwa litakua la uhakika hivyo kupanua uchumi wa Wilaya ya Meatu.
“Twendeni tukafungue matendo kwa vijana wa Tanzania tuwaondoe katika mitazamio ya fikra hafifu na kuwapeleka katika kujitegemea ili wajenge taifa letu na kuondokana na dhana ya umasikini waliyoikumbatia kwa muda mrefu” alisema Mhe. Jenista.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu  Mhe. Anthony Mtaka amemwambia Mhe. Jenista kuwa hatamualika Simiyu kufungua makongamano na warsha za ujasiriamali bali ataendelea  kumualika katika Mkoa wake kwa ajili ya kufungua viwanda vingine vya vijana kwani mkoa umejipanga kuwa na viwanda vya kutosha vitakavyozalisha malighafi zote zinazopatikana Mkoani Simiyu.
Mhe. Mtaka amewaomba wana Meatu na wananchi wote wa Simiyu kuwa na uthubutu wa kubuni miradi endelevu ili waweze kujivunia vya kwao kwani Mkoa umejichagua kuwa pacha wa kutekeleza Ilani ya uchaguzi sambamba na Rais Mhe. John Pombe Magufuli na kuweza kuiongoza nchi kufukia malengo ya Ilani ya Chama tawala kwa vitendo.
Aidha Mwenyekiti wa Meatu Milk Bibi. Lightness Benedictor amesema kuwa mradi umegharimu kiasi cha shilingi 34,903,000 ambapo shilingi 10,000,000 ni michango ya wanachama kutoka kwenye gawio ya fedha za mkopo uliotolewa na Wizara kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kiasi cha shilingi 24,902,000 ni mkopo kutoka kwenye asilimia tano ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya fedha zilizotengwa kuwezesha vijana.
Mradi wa Meatu Milk unatekelezwa chini ya mpango mkubwa wa kiuchumi wa Mkoa wa Simiyu wa kuanzisha bidhaa moja kwa Wilaya moja ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 ya kuwa na Tanzania ya viwanda.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.