Habari za Punde

KAMPUNI YA SBL YASHEREHEKEA KUTIMIZA MIAKA 20,YAZINDUA MUONEKANO MPYA WA BIA YAKE

Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na uongozi wa kampuni ya SBL, ilipokuwa ikitangaza kuanza kwa sherehe maalumu ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. 

Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.

Helene amesema kuwa kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini. 
Pichani kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habaria,wakati kampuni hiyo ikitangaza kuanza kwa sherehe maalumu ya kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.Helene amesema kuwa kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
PIchani kulia ndio muonekano mpya wa bia ya Serengeti ambayo imekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” SBL imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuanza kwa sherehe maalumu kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bia ya Serengeti Premium Lager (SPL) mwaka 1996. Sherehe hizo zinaambatana na uzinduzi upya wa bia hiyo ikiwa katika muonekano mpya.
*************************************************
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa SBL Helene Weesie, amesema mbali na kuonesha mafanikio ya bia ya Serengeti kwa kipindi cha miongo miwilil iliyopita, kampuni ya SBL itatumia kipindi hiki kuwashukuru wateja wake na umma wa Watanzania kwa kuikubali bia ya Serengeti kama chaguo lao la hivyo kuifanya kuwa mingoni mwa bia zinazoongoza hapa nchini.

“Tunawashukuru wateja wetu, wafanya biashara, wasambazaji, mashirika ya sekta binafsi, serikali na wadau wote ambao kimsingi wametusaidia na kuwa nasi katika safari yetu hii ya mafaniko,” amesema Weesie.

Bia ya Serengeti Premium Lager ni ya kwanza kutengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 hapa nchini ikiwa ni ubunifu wa Mpishi Mkuu mtanzania aitwaye Winston Kagusa ambaye alichanganya mbinu ya utengenezaji wa bia za kijerumani na vionjo vya hapa nchini kupata kupata kinwaji hiki kinacopendwa na wengi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, bia ya Serengeti ilizalishwa kwa mara ya kwanza ikilenga kufikia sehemu ndogo maalumu ya soko lakini azma hii ilibadilishwa na kuzalishwa kwa wingi kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji ya bidhaa hiyo jambo ambalo lilisababisha kuanzishwa uzalishaji zaidi katika viwanda vya SBL vilivyoko Moshi na Mwanza. 

Aidha Mkurugenzi huyo ameendelea kusema kwamba katika kipindi chote cha miongo miwili bia ya Serengeti imekuwa na vifungashio vya muonekano tofauti tofauti vinavyoakisi mabadiliko ya kinyakati na mahitaji ya wateja wake. “muonekano mpya tunaouzindua leo hii ni muendelezo wa kielelezo hiki kwamba daima SBL tunajali mahitaji ya wateja wetu na tuko karibu nao, amesema Weesie.

“Tunaona fahari kuzalisha Bia ya Serengeti Premium Lager katika ubora uleule wa hali ya juu katika viwanda vyote vitatu, na huu ni uthibitisho halisi kutokana na kutambuliwa na wateja wetu wa ndani pamoja na medali zaidi ya 10 za kutambulika kimataifa ambazo bia hii imeshinda. Tunaahidi wateja wetu kwamba tutaendelea kuzalisha Serengeti Premium Lager katika ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia vigezo vya ubora vilivyoanishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” amesema Weesie.

Uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Serengeti pia umekuja na kauli mbiu mpya wa kinywaji hicho cha “Taifa Letu. Fahari Yetu. Bia Yetu.” Aidha kampuni hiyo imewakaribisha wateja wake na wadau mbalimbali kutoka sekta za umma na binafsi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 20 ya bia ya Serengeti yatakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.