Habari za Punde

KOCHA MKUU WA YANGA PLUIJM NA WENZAKE KUFUNGASHIWA VIRAGO YANGA

George-Chicken-Lwandamina, aliyetua nchini kurithi mikoba ya Mholanzi, Pluijm.
***********************************
Na Ripota wa Mafoto Blog,Dar
BAADA ya kufungwa mechi moja na kuambulia sare tatu katika mechi zake 10 ilizocheza, timu ya Yanga huenda ikawafungashia virago Viongozi wake wa Benchi la Ufundi akiwemo kocha Mkuu Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi na Wasaidizi wake, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakupenda kutajwa jina lake, alisema kuwa mabadiliko hayoya benchi la ufundi yanatarajia kufanyika hivi karibuni baada ya kuwasili kwa Kocha mpya George Lwandamina, kutoka nchini Zambia.

Aidha imeelezwa kuwa Kocha Pluijm baada ya kukabidhi mikoba kwa kocha huyo Mzambia yeye atabakia kuwa Mkurugenzi wabenchi la Ufundi la Yanga, huku wenzake wakisalia katika nafasi zao iwapo Kocha huyo mpya hatahitaji mabadiliko ya wasaidizi wake.

Habari za chini chini kutoka kwa wadau wa timu hiyo zinasema kuwa huenda Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Bonoface Mkwasa, akarejea kikosini na kupokea kijiti cha Juma Mwambusi kuwa Kocha Msaidizi wa Mzambia huyo, huku Kipa wa zamani Peter Manyika akipokea kijiti cha kipa mwenzake wa zamani Juma Pondamali na kuwa kocha wa makipa.

Hadi sasa Yanga inajumla ya pointi 21 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara wakiwa tayari wamecheza jumla ya michezo kumi wakiwa katika nafasi ya pili wakishinda mechi sita wakiongozwa na mahasimu wao Simba wenye jumla Pointi 31.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.