Habari za Punde

KOCHA PLUIJM AJIUZULU NA KUWAAGA RASMI WACHEZAJI WA YANGA LEO, AGOMA KUWA MKURUGENZI YANGA

Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
BAADA ya kuwasili kocha mpya wa Yanga kutoka Zambia, hatimaye leo Kocha Mkuu wa Yanga Hans Der Pluijm, ametangaza rasmi kujiuzulu mwenyewe wadhifa wake huo na kuwaaga rasmi wachezaji wake na wasaidizi wake wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika leo asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao na JKT Ruvu unaopigwa kesho, jijini.

Kocha huyo amefikia maamuzi hayobaada ya kuenea tetezi za kuwasili kwa kocha mpya Mzambia kwa ajili ya kurithi mikoba yake bila Uongozi wa Klabu hiyo kumshirikisha jambo ambalo limeonekana ni dharau ya viongozi na kumchoka ndani ya Klabu hiyo.

Aidha imeelezwa kuwa Kocha huyo pia ameugomea uongozi wa Yanga kusalia ndani ya Klabu hiyona kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, akisema kuwa hakufurahishwa na jinsi uongozi ulivyochukua maamuzi ya kuleta Kocha mpya bila kumtaarifu, huku akiwaeleza wachezaji wake kuwa ameamua kuondoka nchini na kurejea kwao, akiwa na matarajio ya kupata timu ya kufundisha kulingana na CV zake.

Hata hivyopamoja na Kocha huyo kuweka wazi kuwa anaondoka nchini na kurejea kwao lakini tayari tetesi zimeenea kwamba Kocha huyo huenda akatua Azam kotokana na habari zilizochini ya kapeti kuwa Azam wameonyesha nia ya kumhitaji Kocha huyo.

Tayari za chini ya Kapeti zimeenea kuhusu Safu ya Uongozi mpya wa Klabu hiyo baada ya kuondoshwa Pluijm na Wasaidizi wake wote, ambapo Kocha mkuu atakuwa ni Mzambia Lwandamina atakayesaidiwa na wazalendo Charles Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.