Habari za Punde

KUMBUKUMBU YA MIAKA 17 YA MWALIMU NYERERE

Leo Tanzania inaadhimisha miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia. Kitaifa maadhimisho haya huambatana na sherehe za kuzima Mwenge na kwa mwaka huu itafanyika katika mkoa wa Simiyu.
Akiwa mgombea wa Urais mwaka jana Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere huko kijijini Mwitongo, Butiama, mkoani Mara akiwa ameongozana na ujumbe wake.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiongea na viongozi mbalimbali waliomtembelea Butiama
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa na Waziri Mkuu wa India Indira Ghandi pamoja na Rais Kenneth Kaunda wa Zambia, Rais Josef Tito wa Yugoslavia, Milton Obote wa Uganda na Sir Seretse Khama wa Botswana
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akikumbatiana na aliyekuwa mgombea Urais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya matokeo kutoka na Mhe. Benjamin Mkapa kutangazwa mshindi kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu mwaka 1995.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.